1000126984


WAZIRI wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa ameiagiza bodi ya wahandisi (ERB) kuhakikisha inafanya mapitio ya sheria yao ili kuona kama inamapungufu kwa ajili ya kuiwasilisha bungeni ili iweze kufanyiwa marekebisho.


Bashungwa ametoa maagizo hayo leo Mei 23,2023 jijini Dodoma , wakati akuzungumza kwemye mkutano wa 6 wa mafundi sanifu.

Amesema lengo la kuchukua hatua, ni kulinda na kurejesha hadhi na heshma ya wahandisi wazawa nchini

1000125964

"ERB nimewambia mara kadhaa kuwa kama sheria inamapungufu basi muilete ili tuweze kuipeleka bungeni na kuifanyia marejebisho," amesema Bashungwa

Pia amewataka wahandisi kuhakikisha wanawashughulikia wahandisi ambao wanaishushia hadhi na heshima taaluma hiyo nchini huku akiwataka kuwaripoti ili waweze kuwachukulia hatua hadharani na kuwa mfano.


"Wasikubali kuona watu wachache wasiokuwa waaminifu na waadilifu wanawavunjia heshima na kuwashushia hadhi ya taaluma hiyo ya uhandisi nchini "amesisitiza Bashungwa

1000125972

Amesema Serikali inawaamini na inatambua kuwa wapo wahandisi na mafundi sanifu wazawa ambao wanafanya kazi na wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha viwango na ubora.

"Mkakati wa serikali wanakamikisha mpango wa kusaidia wakandarasi wazawa, eti itokee TANROADS anakazi halafu wasimpe kijana wa kitanzania huyo atakuwa hajitaki mana sitomuelewa,"amesema
Bashungwa pia aliagiza mafundi sanifu wasajiliwe kama yalivyo matakwa ya kisheria

"Ni vizuri mafundi sanifu wajisajili kwa wingi ERB Ili kunufaika na fursa ambazo zinatolewa na serikali na kuhusu Kupanda cheo wajiendeleze kielimu

Kuhusu usajili wa wakandarasi aliagiza CRB ifuatilie taarifa kupata na kutoa taarifa mpya za wakandarasi Ili kupandisha daraja wale ambao wanakuwa na kufanya vizuri na kuwashusha wale ambao wanafanya vibaya.

Waajiri wawachagize na kuwasaidia mafundi sanifu katika maeneo yao ya kazi, na kuhakikisha fursa walizonazo zinawapa thamani wanayoitarajia.

Waziri Bashungwa amesema kuwa Mafundi sanifu ni jukwaa muhimu linalohitajika kwa maendeleo ya nchi hivyo waendelee kujituma na kujiamini kwenye matumizi ya teknolojia Ili kujitoa kwenye utegemezi wa teknolojia kutoka nje

Pia aliwataka kubuni teknolojia zenye mahitaji ya ndani ya nchi kwani ukuaji wa teknolojia duniani mataifa hubuni vitu ambavyo vina anufaa kwa nchi zao kw ajili ya Maendeleo

"Nawasihi bunifu za Teknolojia zisiishie kwenye karakana bali zitangazwe kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza soko la ajira.

1000125993

"Ipo Miradi mingi inatekelezwa kwenye halmashauri lakini uwiano wa Mhandisi na Miradi hauko sawa Mhandisi mmoja ana Miradi zaidi ya hamsini lakini mafundi sanifu hawapo,"amesema waziri Bashungwa

Awali msajili wa Bodi ya ERB, Mhandisi Bernard Kavishe , amesema madhumuni ya kukutanisha mafundi sanifu ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kada hiyo ikiwemo kukumbushana kuzingatia sheria na kanuni zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ERB Dk. Menye Manga amesema mafundi sanifu ni kada muhimu kwa maendeleo ya nchi hasa katika sekta za Ujenzi na viwanda.

1000125976
1000125945
1000125968
1000125985
1000125989
Share To:

Post A Comment: