Mheshimiwa Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Mhe. Silvino Augusto José Moreno, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Msumbiji kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Jijini Maputo.

Katika mkutano huo, Viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ili kufanikisha ushirikiano katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji.

Vilevile, Viongozi hao wamekubaliana kutafuta mbinu na mikakati mahsusi ya kuongeza  kiwango cha biashara baina nchi hizi ili kiende sambamba na uhusiano wa kindugu, kihistoria na kijiografia baina ya nchi hizi. 

Moja ya maeneo yaliyopendekezwa ni kuanzisha  Jukwaa la Pamoja la Biashara litakalowakutanisha Wafanyabiashara na wadau wengine muhimu ili kubadilishana uzoefu, kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na kubaini namna ya kunufaika nazo.


Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Maputo.






Share To:

Post A Comment: