Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amewaasa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kutembelea Vifua mbele katika kumsemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta Maendeleo katika Taifa letu.

 Ndugu Vijana wenzangu tutembeee kifua mbele kumsemea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani kazi zake anazozifanya tunaziona"

"Ndugu zangu Cha Mapinduzi hakijawahi kukosea katika kuchagua na kuteua Viongozi hivyo tuna kila sababu ya kuhabarisha Umma juu ya Utekelezaji Kishindo wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020 uliofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upande wa Tanzania Bara lakini pia Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa upande wa Zanzibar". Alisema Komredi Jokate.

Share To:

Post A Comment: