Ashrack Miraji Kilimanjaro 

Mbunge wa jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo,amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika sekta za elimu, maji, afya na miundombinu ya barabara ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.


Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mwanga,wakati wa uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendelea wilayani hapo, Tadayo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia inaendelea kutekeleza mipango ya maendeleo ambapo Mwenge wa Uhuru 2024 umetembelea miradi Sita  ambayo mingine imeshazinduliwa na mingine kuwekewa jiwe la Msingi.


Amesema Rais amewawezesha wananchi wa Mwanga kupata huduma stahiki zitakazosaidia kupunguza changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao na kwamba wanamshukuru Kwa mapenzi yake ya dhati kwa kuwadhamini na kuwapatia huduma mbalimbali za kimaendeleo kama vile maji,afya,elimu,umeme n.k


Tadayo amesema kuwa wakati Mwenge wa Uhuru ulipozindua mradi wa maji unaohudumiwa na Ruwasa ambao ni miongoni mwa miradi Sita iliyotembelewa na mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 kwenye wilaya hiyo.


"Ukweli mradi huu wa maji wa Kata Kivisiniambao Kijiji cha kwa nyange unahudumia vitongoji vitatu vyenye wakazi zaidi ya 3000 unakwenda kuwa chachu ya maendeleo kwa wakazi wa hapa kutokana na jiografia ya wiilaya yetu kwamba changamoto kubwa ni maji"


"Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameona uchungu Kwa wakazi hawa na kuleta kiasi hicho Cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji mpaka leo hii Mwenge wa Uhuru mwaka huu umekuja na kupunguza kero ya ukosefu wa maji Kwa Wananchi na mimi kama kiongozi nitaendelea kupaza Sauti yangu "


Sambamba na hayo yote pia mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zilizindua bweni la shule ya secondary Asha Rose Migilo ,mradi wa kikundi Cha vijana Wajasiliamali (bodaboda) pamoja na Klabu ya Kupambana na Rushwa na kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa zahanat ya Kwa Nyange pamoja na ujenzi wa barabara ya Usangi wilayani hapo.


Tadayo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mwanga,pia kutoa salama Kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Ndugu Godfrey Mnzava kumfikishia kwa Mhe Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan salamu za upendo kutoka kwa wananchi wa Wilaya hiyo.


Ikumbukwe kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024 ni "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".




 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: