Na Mapuli Kitina Misalaba

Wakristo na jamii kwa ujumla wameshauriwa  kujiwekea utaratibu wa kuwa na kumbukumbu za matukio muhimu katika maisha yao ili kutengeneza maisha bora yajayo.

Hayo yamezungumzwa leo April 1,2024 na Mchungaji Christian Kubena  wa Kanisa la Tanzania Assembless of God T.A.G Shinyanga, wakati akihubiri kwenye ibada ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo Nchini.

Mchungaji Kubena  amesema ni muhimu kila mmoja kujiwekea utaratibu wa kuwa na kumbukumbu ya matukio muhimu ili kutengeneza maisha bora yajayo.

“Leo tumekuwa na maadhimisho haya ya Miaka 85 tangu tuanze, tukio hili linaweza kuwa na tafsiri mbalimbali lakini iko tafsiri iliyoyakweli ambayo hii inathibitishwa hata na mamlaka ya maandiko matakatifu ya neno la Mungu  na ukisoma kitabu cha kumbukumbu la tolati sura ya 16 mstari ya kwanza hadi wa 17 anaelezea pale, Mungu anatoa maelekezo ya mambo ambayo watu hao wanapaswa kukumbuka”.

“Mwanadamu anapokumbuka kila kumbukumbu ina nguvu kwa sababu kila jambo linalotokea kwenye maisha ya mwanadamu huwa lina kusudi na linamajira kwa kusema hivyo kumbukumbu ulizonazo juu ya matukio mengi ya maisha yako Mungu ameziruhusu zinaweza kuwa ni fursa ya kuwa na kesho nzuri zaidi, mtu asiyekuwa na kumbukumbu au asiye kumbuka mara zote huwa hawezi kupiga hatua za maendeleo mfano mzuri tu mtu anakumbuka vile alivyoteseka kwenye familia yao Baba alifariki au Mama alifariki wakawa yatima watoto hao wanapokuwa watu wazima hawawezi kuchezea mali”.amesema Mchungaji Kubena

Akisoma taarifa iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa la T.A.G Rehoboth Christian Centre -Shinyanga katibu wa kanisa hilo Bi. Gilselda Kasili ameelezea historia fupi ya ambapo ametaja mwenendo na maendeleo ya Kanisa hilo.

Ameeleza kuwa kanisa hilo limeendelea kuifikia jamii ambapo limefanikiwa kutembelea magreza, hospitali pamoja na kuchangia damu salama katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 85.

“Tanzania Assemblies of God ni Kanisa lililosajiriwa tarehe 21/10/1981 chini ya sheria ya societies ordinance yam waka 1954 na kupewa namba ya usajiri SO/ 6246, kanisa hili lilitokana na uamsho mkubwa ulioanza huko mtaa wa AZUSA, California (Marekani), mwanzoni mwa karne iliyopita ya ishirini”.

“Mwanzilishi wa kanisa hili nchini Tanzania ni mmisionari ndugu Paul Deer Mwaka 1939 wakati huo ikiitwa Tanganyika hapo ndipo hesabu za umri wa kanisa letu hapa nchini zinapoanzia, hivyo kutupa uhalali wa kusherehekea miaka 85 ya uhai wa Tanzania Assemblies of God Mwaka huu wa 2024”.

 “Historia inatuonesha kuwa katika miaka ya mwanzo kanisa lilisimamiwa na  wamishenari wa  kimarekani, wachungaji wa kiafrika  wakati huo, Yohana Mpayo (Marehemu) na  Petros, walikuwa maaskofu  chini ya Assemblies of God Mission”.

“Kanisa liliendelea kuongozwa katika mfumo huo wa kuongozwa na  wamisionari hadi  mwaka 1967, na Mwaka huo wa 1967, uongozi wa Assemblies of God Mission, uliamua kulikabidhi kanisa kwa uongozi wa wenyeji na Mchungaji Immanuel Lazaro, alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mtanzania wa kuongoza Tanzania Assemblies of God (TAG)”. amesema Kasili

“Lengo kuu la kuanzishwa kwa kanisa hili ni kuwafikia  watu wote kwa injili iliyo hai, iletayo wokovu na kuleta uamsho mkubwa wa Bwana wetu Yesu Kristo hapa nchini, kwa hapa Mkoani Shinyanga liliingia  Mwaka 1968 na hadi Mwaka huu kanisa lina miaka 56 Mkoani hapa,

“Malengo ya kanisa hili ni kulitimiza kusudi lililokuwepo ndani ya kristo la kuwafikia wengine, na hili kulitimiza hili lengo tumeweza kulifikia kwa njia mbali mbali ikiwemo; makongamano,mikutano ya injili, semina,ushuhudiaji wa mtu mmoja mmoja na wa nyumba kwa nyumba, njia ya sinema.

Tunatambua kuwa Mungu ametuweka hapa kama kanisa ili kuleta mabadiliko chanya kiroho, kiakili na kimwili kwa jamii inayotuzunguka. Kanisa kwa kushirikiana na Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ‘Compasion International’, tunawahudumia watoto walio katika mazingira magumu katika nyanja ya kiroho, kimwili, kijamii na kiakili. Hadi mwaka huu 2024 kituo kimeishahudumia jumla ya Watoto 250”.

“Mbali na kituo hiki kanisa tumeendelea kuifikia jamii inayotuzunguka kwa ajili ya kukutana na mahitaji yao ya kimwili na kiroho pia, wa kipindi hiki cha miaka 13 ya moto wa uamsho tumefanikiwa kutembelea Magereza, Hospitali pamoja na kuchangia damu salama katika hospitali yetu ya Manispaa ya Shinyanga”.

“Kanisa letu linawafikia wengine kwa njia ya mtandao ambapo tunarusha ibada zetu na huduma zetu mbalimbali kwenye mtandao wa ‘facebook’ na you tube ikiwa ni pamoja na ibada mubashara, lengo likiwa ni  kuwafikia watu wengi na hasa watumiaji wa mitandao hiyo ndani na nje ya Tanzania”. amesema Kasili

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amelipongeza kanisa hilo la T.A.G kwa  hatua hiyo ya mafanikio.

Pamoja na mambo mengine kanisa la Tanzania Assembless of God (T.A.G) Rehoboth Christian Centre -Shinyanga leo Aprili mos limefanya maandamano ya amani na kuchangia damu salama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Mchungaji Christian Kubena  wa Kanisa la Tanzania Assembless of God T.A.G Rehoboth Christian Centre –Shinyanga akihubiri kwenye ibada ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini.

Katibu wa kanisa la T.A.G Rehoboth Christian Centre -Shinyanga Bi. Gilselda Kasili akisoma taarifa fupi ya kanisa hilo.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza leo Aprili mos ambapo amelipongeza kanisa hilo la T.A.G kwa  hatua hiyo ya mafanikio.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza leo Aprili mos ambapo amelipongeza kanisa hilo la T.A.G kwa  hatua hiyo ya mafanikio.






Mchungaji Christian Kubena  wa Kanisa la Tanzania Assembless of God T.A.G Rehoboth Christian Centre –Shinyanga akihubiri kwenye ibada ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini.

TAZAMA VIDEO
Share To:

Misalaba

Post A Comment: