Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka Maafisa Habari nchini kuwa wabunifu,weledi na kufanya kazi kwa uweledi ili kukuza tasnia ya Habari sanjari na kuisaidia serikali katika utendaji wake.
Ameyasema hayo katika hafla ya kukabidhi tuzo za umahiri kwa maafisa Habari na Uhusiano zilizoandaliwa na Taasisi ya Public Relations Society of Tanzania(PRST) ambapo Shirika la la Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA)kupitia Idara ya Mawasiliano imeshinda tuzo ya Umahiri katika Mawasiliano ya Umma.
Aidha amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano na kwamba wanahitajika Maafisa Uhusiano wa kisasa zaidi ili tasnia hiyo iwe na tija kwa serikali.
Hata hivyo amewataka wasimamizi wa tuzo hizo wasitoe tuzo kwa upendeleo ili vigezo na masharti yazingatiwe.
“Naamini tuzo hizi zitaidia kuboresha kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na waliokosa tuzo wasife moyo bali itawapa ari ya kufanya vizuri mwakani”alisema Mahundi.
Kwa upande wake Mobhali Matinyi Msemaji Mkuu wa Serikali amesema hii ni fursa kwa Maafisa Uhusiano kufanya kazi zao bila kuwategemea Waandishi wa Habari kutoka nje ya ofisi na utaratibu huo utaharakisha utendaji kazi wa kila siku.
Hii ni kazi yake ya kwanza kufanywa na Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi tangu apate uhamisho kutoka Wizara ya Maji
Post A Comment: