1000003747


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) itaendelea kukiimarisha Kitengo cha Usimamizi wa Miradi kutoka TANROADS (TECU) ili kiweze kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi kwa gharama nafuu.

Bashungwa ameeleza hayo leo Aprili 10, 2024 Mkoani Songwe wakati akizungumza na Watumishi wa TANROADS na kueleza kuwa mpaka sasa miradi mingi inayoendelea kutekelezwa inasimamiwa na wahandisi washauri kutoka nje ambapo tumekuwa tukipoteza ajira nyingi za watanzania.

“Tunaenda kuimarisha Kitengo cha TECU kiwe kikubwa, kupitia TECU tuweze kusimamia miradi yetu na tuone namna ya kutumia Wataalam waliostaafu ili waweze kutoa uzoefu kwa wahandisi vijana katika miradi watakayoisimamia”, amesisitiza Bashungwa.

1000003595

Bashungwa ameeleza kuwa Kitengo cha TECU kikiimairishwa kitatoa fursa kwa wahitimu wa Kada ya Uhandisi kupata uzoefu pamoja na ajira kupitia miradi itakayosimamiwa na TECU.

Aidha, Bashungwa amewataka watumishi wa TANROADS kuendelea kuwa wazalendo kwani wanasimamia miradi inayogharimu fedha nyingi hivyo lazima waone uchungu na fedha zinazotumika.

“Tunapokuwa kwenye usimamizi niwaombe sana kila mtumishi awe na uchungu wa fedha kubwa ambazo ni kodi za watanzania wenzetu, lazima mjue kuwa watanzania wanatutegemea sisi na wanahitaji miundombinu tunayoisimamia”, amesema Bashungwa.
1000003749
1000003748
Share To:

Post A Comment: