Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amesema  Mikoa ya Kanda ya Kusisni Mtwara, Lindi na Ruvuma ni wanufaika wakubwa wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo ndani ya kipindi cha Miaka 3 ya Uongozi wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

 "Ndugu Vijana wenzangu; ninyi wote ni mashahidi ndani ya kipindi cha Miaka 3 Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mmenugaifaika kwa ming ya Maendeleo"

"Pamoja na mambo mengi mazuri yaliyofanywa na Serikal yetu ndani ya Mikoa yetu hii katika sekta ya afya, miundombinu, Utalii, Elimu Lakini jambo kubwa na la kipekee sana ni Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mikindani Mkoa wa Mtwara. Hospitali ambayo  inahudumia Wananchi wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 15.8 haya yote ni Mapinduzi Makubwa katika Sekta ya Afya ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita".


Share To:

Post A Comment: