Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imewanoa maofisa na wahifadhi udhibiti wanyamapori zaidi ya 35 katika Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya Enduiment (WMA) iliyopo Kata ya Tingatinga wilayani Longido juu ya udhibiti wa dawa za kulevya wilayani Longido.

Kwamujibu wa Ofisa Elimu kutoka DCEA Kanda ya Kaskazini,Shabani Miraji amesema elimu hiyo ni muhimu kwa maofisa hao kwani wakati fulani hukutana na kuwadhibiti wahalifu wanaosafirisha dawa za kulevya hususani mirungi na bangi kupitia vipenyo vya mpakani kwa kutumia njia za panya kuelekea mjini Arusha.

Shabani amesema elimu juu ya madhara ya matumizi dawa za kulevya, udhibiti wa usafirishaji haramu wa dawa za kulevya na sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya itakuwa chachu kwa maofisa hao kuimarisha mapambano katika maeneo yote ya hifadhi ili wahalifu wa dawa za kulevya wasiweze kusafirisha dawa za kulevya kupitia maeneo hayo yenye vipenyo.

Share To:

Post A Comment: