Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amemtaka mhandisi anayesimamia mradi wa maji MISISI ZANZIBAR kuruhusu maji masaa24 na kuwaunganishia wananchi kwenye maeneo yao ili kufurahia na huduma hiyo.

Utaratibu wa kupeleka maji vijijini ni wa tangu Rais Samia akiwa makamu alipoazisha kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani na kuhakikisha maji yanafika kila sehemu. Waziri Mkuu MAJALIWA ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa maji MISISI ZANZIBAR katika kata ya sazira Halmashauri ya Mji wa Bunda Majaliwa amesema mradi huo wa maji utaendelea kuongezewa maji kutoka ziwa victoria.

Majaliwa amewasisitiza wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali kwani inaendelea na mikakati ya kutatua changamoto ya maji katika maeneo yote ambayo yanatakiwa kufikiwa na huduma hiyo. Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amesema kuwa miaka ya nyuma viongozi wengi waliofika katika mji wa Bunda walikuwa wakipokelewa na ndoo za maji, kutokana na changamoto ya kutokamilika kwa miradi ya maji na fedha zilizokuwa zikitolewa zinaliwa na watu bila mafanikio.

Aweso amesema kuwa wananchi wa Bunda wanahitaji lita milioni 9 na mradi wa Chujio wa Nyabehu unauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 15 na Wizara ya Maji ipo tayari kusapoti kuhakikisha kila maeneo wanapata maji safi. Amesema ni haki ya kila mwananchi kupata huduma ya maji na amekemea kubabikizia mteja bili ya maji ,atozwe bili kutokana na matumizi yake na wizara inatarajia kutumia mfumo wa luku kwa ajili ya malipo ya maji hii ni kutokana na malalamiko ya ulipaji bili.

Amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWASSA),Bi. Esther Gilyoma kwa kazi nzuri pamoja na kukamilika kwa mradi mkubwa wa kusambaza maji wa Nyabehu ambao kukamilika kwake ilikuwa ni changamoto kubwa lakini kwa sasa unasubiri kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa Waziri Mkuu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mjini Bunda Bi.Esther Gilyoma amesema kuwa mradi wa Misisi Zanzibar umetekelezwa kwa force account na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 700 na kusimamiwa na wataalam wa ndani na utakaoenda kunufaisha wakazi zaidi ya 7000. Mwisho, Mheshimiwa Aweso amesema kuwa serikali imetoa pesa nyingi na inaendelea kukarabati na uboreshaji wa uchakavu wa miundombinu ya maji.

Share To:

Post A Comment: