MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge ameunga mkono juhudi za chama hicho Taifa ya kuanzisha CCM APP baada ya kugawa simu zitakazowezesha makatibu wa UWT wilaya kusajili kwa kutumia Application ya CCM ambayo ndani yake ina kipengele cha UWT.

 

Hatua ya Mbunge huyo kugawa simu hizo ni kuhakikisha wanachama wanasajiliwa kieletroniki ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ili kuweza kupata ushindi wa kishindo.

 

Akizungumza wakati wa Baraza la Kuu la Kawaida la UWT Mkoa wa Tanga wakati alipokwenda kutoa taarifa za kazi zake katika utekelezaji wa ilani ya CCM tokea alipopewa ridhaa ya kuwa Mbunge kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa huo

 

Ambapo alisema mpango wa CCM App wao kama UWT Mkoa wa Tanga wanaiunga mkono kwa kuhakikisha wanasajili wanachama wao na kwani ndio msingi imara ambao utawawesha kuendelea kufanya vizuri kwenye chaguzi.

Share To:

Post A Comment: