NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema Serikali itaendelea kuunga mkono michezo ya aina yote kuanzia ngazi ya chini ili kuwatia moyo wanamichezo wanaoanza na wale walioko kwenye tasnia hiyo.

Mwinjuma ‘Mwana FA’ ameyasema hayo usiku wa kuamkia Januari 02, 2024 baada ya kushuhudia mapambano ya ngumi yanayojulikana kama “Usiku wa Mawe Hananasif” yaliyofanyika Kinondoni, Dar es salaam.

Aidha, ametoa rai kwa wawekezaji kutoka sekta binafsi wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika mchezo wa ngumi ili kuwapa nafasi mabondia kuonekana.

“Sisi tumeelekezwa na Rais kushuka chini kabisa kuhakikisha tunasimamia michezo yote, kuhakikisha kwamba tunavumbua, tunavilea na kuvitunza vipaji vingi kwenye michezo inayofanyika hapa nchini” amesema Mwinjuma.

Share To:

Post A Comment: