Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea kwenye tamasha la utalii Wilayani Same Mkuu wa Wilaya hiyo amesema tamasha hilo litaibua fursa mbalimbali za ajira kwa wananchi wa Wilaya hiyo pamoja na maeneo mengine.

Tamasha hilo ambalo limepewa jina la SAME UTALII FESTIVAL linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 22-24 February mwaka huu na litafanyika katika viwanja vya stendi ya mabasi mjini Same.

Kuelekea kwenye tamasha hilo Mkuu wa Wilaya hiyo ya Same Mkoani Kilimanjaro Kaslida Mgeni amesema pamoja na kuwa ni tamasha la utalii ila litaibua fursa mbalimbali za ajira pamoja na uwekezaji ndani ya Wilaya hiyo.

Kaslida awataka wananchi wilayani hapo kutumia nafasi hiyo katika kutangaza bidhaa zao hususani bidhaa za asili ilikuwavutia watalii watakaofika kwenye tamasha hilo.
“Tume andaa tamasha hili kubwa la utalii Wilayani same lengo letu ni kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr.Samia Suluhu Hassan ambaye hivi karibuni amezindua filam ya Royal Tour kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii Nchini na tumeona matokeo yake chanya hivyo basi kama Wilaya tumeamua kumuunga mkono Rais wetu kwa kufanya tamasha hili ambalo litaibua hisia za watanzania walio wengi”
“Alisema DC Kaslida “.

Akizungumza kuelekea kwenye tamasha hilo Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Emmanuel Moirana amesema kupitia tamasha hilo wanatarajia kupata ongezeko kubwa la watalii wa ndani na nje.

Moirana amesema kwa mwaka wa fedha 2022-2023 kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii ndani ya hifadhi hiyo Kutoka watalii 2000 kwa mwaka 2020 hadi kufikia watalii zaidi ya 7000 kwa mwaka 2022-2023 ikiwa ni baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa utalii wa Faru ndani ya hifadhi hiyo.

Happness Kiemi na Samweli Mpaning’ombe maafisa utalii Kutoka hifadhi ya Taifa Mkomazi na msitu asilia wa Chome wamesema kupitia tamasha hilo watanzania na wageni Kutoka nje ya Nchi wataweza kufurahia vivutio mbalimbali vinavyopatikana kwenye hifadhi hizo.

Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same kwakushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameandaa tamasha kubwa la utalii litakalofanyika kuanzia tarehe 22-24/02/2024 likiwa na lengo la kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii Wilayani hapo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye hivi karibuni amezindua filam ya Royal Tour.

Mwisho.

Share To:

Post A Comment: