Waziri wa Utamaduni sanaa na michezo Damas Ndumaro amewataka maafisa habari wa serikali kutangaza miradi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili wananchi wajue ikiwemo kujibu hoja za uongo zinazotolewa na watu dhidi ya serikali .

Akifungua Mkutano wa siku tatu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Dk,Damas Ndimbaro kwaniaba ya Naibu Waziri Mkuu,Doto Biteko.

Alisema maofisa hao wanawajibu mkubwa wakutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili watu waone ukubwa wa kazi zinazofanywa na serikali katika nchi hii

“Baadhi ya watu hawaoni ukubwa wa katarasi nyeupe ulivyo sasa ni wajibu wenu kueleza kazi zinazofanywa na serikali ikiwemo kujibu hoja za uongo dhidi ya serikali lazima mjue kujibu fitna na zengwe”

Alisema hata serikali inapigwa fitna sasa ni kazi yenu kujibu fitna na zengwe kwani hivi sasa zama za teknolojia ya habari imekua na ni nzuri ila inachangamoto zake kupitia mitandao ya kijamii.

Alisema mojakati ya changamoto kubwa iliyoletwa na mitandao ya kijamii haijui ni nani mtoa habari na nani anayepaswa kujua hii ni habari hivyo tumieni changomoto hizi kwaajili ya kujibu hoja na lazima mafunzo ya mara kwa mara yatolewe ya matumizi ya mitandao ya kijamii

“Ongezeni ubunifu zaidi,msifanye kama jana kazi zenu maafisa habari ili muweze kupambana zaidi na kuipambania serikali ”

Alitoa rai kwa waandishi wa habari vyombo vya serikali na maafisa habari kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uzalendo,weledi na ubunifu pale taarifa zinavyoandikwa

Alitoa maelekezo kwa waaajiri wote wasioweza kuleta maafisa habari kushiriki mkutano huo watoe maelezo kimaandishi na ifikapo mwakani Maafisa wote wa serikali na wasio wa serikali wajiunge na chama hicho

Alisema treni ya majaribio ya umeme imeanza kazi kwa majaribio ingawa kulikuwa na kebehi nyingi sana lakini treni imeshaanza kazi hivyo serikali inafanya kazi kwa vitendo

Aliwasihu maafisa hao kujiunga kwa pamoja kutetea serikali pale jambo linapotokea badala ya kuachia wizara husika pekee kutoa ufafanuzi ikiwemo kutoa hamasa kwa wananchi kujua umuhimu wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwemo utangazaji wa miradi ya kimkakati ya serikali

Huku Msemaji Mkuu wa Serikali,Mobhare Matinyi alisema baadhi ya halmshauri hazina maafisa mawasiliano wa serikali badala yake maofisa Tehama ndio wanaongoza kitengo hicho hali inayokwamisha hali ya wananchi kupata habari.

“Halmashauri 180 zilizopo nchini lakini inashangaza kuona baadhi yao siwezi kutaja idadi hazina maafisa habari na hawajui maana ya habari na ukiuliza sababu gani hakuna maafisa habari unajibiwa majibu yasiyorithisha”

Lakini pia kwenu maafisa mawasiliano ya serikali wapeni nafasi nao wananchi wazungumze kuhusu mambo mbalimbimbali yanayowasibu ila pia ni lazima sasa halmashauri ziajiri maafisa habari ili waweze kusemea vema serikali na wananchi kupata habari zaidi

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari na Teknolojia na Mawasiliano, Selestine Kakere alisema wizara inatekeleza kutangaza sera,kanuni na taratibu ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ambapo kazi za serikali kwa Umma zinafanyika kupitia mitandao ya kijamii,radio na luninga

Alitoa rai kwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya ambao mikoa yao Haina maofisa habari wafanye hima kuajiri maofisa habari katika mikoa yao stahiki

Alisema mikoa 14 imepata fursa ya kutangaza miradi mbalimbali ya serikali huku zoezi hilo likiwa linaendelea ikiwemo uwekaji misingi ya uhuru wa vyombo vya habari sanjari na kushamiri kwa idadi kubwa ya vyombo vya habari ikiweo magazeti ,radio na televisheni za mitandao,blogu .

Alisema uwepo wa baadhi ya Wanahabari wengine wasio na weledi na sifa za wanahabari lakini bodi ya ithibati ipo katika hatua ya uanzishwaji ili kusaidia kuimarisha weledi katika sekta ya habari nchini huku baadhi ya taasisi za mawasiliano kwa umma baadhi hazitekelezi majukumu yake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Joshua Nassari alisema ushirikoshwaji wa maofisa mawasiliano ni chachu ya kutoa taarifa kwa umma na kuongeza kuwa wamepokea agizo lakila halmashauri kuwa na maofisa habari na mikoa kwa ujumla

Awali Kaimu Mwenyekiti wa TAGCO, Karim Meshack alisema chama hicho kitaendelea kuhakikisha kinawunganisha maafisa habari kujadili mambo mbalimbali sanjari na kujifunza mbinu mbalimbali za teknolojia za upashanaji habari.

Share To:

Post A Comment: