Watu wote tunatambua ya kwamba Mkoa wa Singida upo katikati ya Tanzania Bara na Mji wake Mkuu ni Singida na ni njia panda muhimu kwa usafiri wa barabara kwenda Kaskazini, Magharibi, Kusini na Mashariki.

CCM chini ya Mwenyekiti wake Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatambua Wakazi wengi wa Singida shughuli zao za kiuchumi ni pamoja na kilimo ambacho huajiri wastani wa asilimia 86% ya wakazi wote. Mazao ya kipaumbele kwa upande wa chakula ni uwele, mtama, mihogo na viazi vitamu na kwa upande wa mazao ya biashara ni alizeti, vitunguu, pamba na ufuta. Shughuli nyingine za uzalishaji mali ni ufugaji, uchimbaji mdogo wa madini, viwanda vidogo na biashara.

Sasa kwa kutambua hilo, CCM imemtuma Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda kupitia ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back kufika katika kuendelea kueneza sera za CCM, kufuatalia na kujionea namna ya utekelezaji wa Ilani Pamoja na kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.

Usipange Kukosa, Wananchi wote wa Singida tukutane leo tarehe 25 Januari, 2024.










Share To:

Post A Comment: