Mtoto Khalfan Gideon wa mkoani Kigoma leo Januari 28, 2024 amefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma – Maweni na kuanza kupatiwa matibabu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Maweni Dkt. Stanley Binagi amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ugonjwa wa Khalfan kimeanzia katika genetics tangu akiwa tumboni.

Amesema kwa sasa wamenza kumpatia tiba za awali mtoto huyo wakati wanafanya utaratibu wa kuchukua sampuli za ngozi kwa ajili kuotesha ili kujua undani wa tatizo na hatimaye kumpatia tiba stahiki.

Mapema hii leo, Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amefika hospitalini hapo kumjulia hali mgonjwa huyo na kuwaagiza madaktari kuchukua hatua za haraka katika matibabu yake ili aweze kurudi shule kuendelea na masomo.

Tunalishukuru Shirika la Habari Tanzania (TBC) kwa kuonesha picha ya video ikimuonesha mtoto Khalfan Gideo akiomba msaada wa matibabu kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais.

Wizara inatoa wito kwa jamii kuwapeleka watoto wenye changamoto za kiafya mapema Hospitalini kwa ajiili ya kupata matibabu na kutowafungia ndani.

Share To:

Post A Comment: