Mahakama ya Wilaya ya Mbulu imemhukumu Melkiadi Zakaria Tlehema aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Hayloto kata ya Nambris, Wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara.

Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa makosa mawili ambayo ni Ubadhirifu na Matumizi Mabaya ya Madaraka, makosa hayo ni kinyume na kifungu cha 28 na kifungu cha 31cha Sheria Ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya Melkiadi Zakaria Tlehema, shauri la Uhujumu Uchumi Na 03/2023, imetolewa chini ya Mhe.Vitalis Eusebius Kapugi, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbulu – Machi 2, 2024.

Mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya shilingi 200,000/= au kwenda jela miezi mitano. Pia mshtakiwa ametakiwa kurejesha fedha alizofanyia ubadhirifu kiasi cha shilingi 1,869,500/=.

Mshatikiwa alifanya ubadhirifu kwenye fedha hizo kupitia makusanyo ya fedha za wananchi kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Hyloto.

Hata hivyo, Mshtakiwa amelipa faini na kurejesha kiasi cha fedha alichofanyia ubadhirifu hivyo ameachiwa huru.

Share To:

Post A Comment: