1000683310


Na Okuly Julius - Dodoma

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka Watumishi katika Sekta ya Afya kuepuka kuwa kikwazo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo ikiwemo ujenzi wa vituo binafsi za Afya.


Amesema sekta binafsi imesaidia kwa kiwango kikubwa kuipunguzia Serikali mzigo hasa katika upande wa ajira kwani vijana wengi wameajiriwa ,ikizingatiwa serikali haina uwezo wa kuajiri watanzania wote


Dtk. Mollel ameyasema hayo Machi 27,2024 wakati akifunga Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi uliofanyika Jijini Dodoma kwa muda wa siku Tatu ambapo washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wameshiriki katika kuchangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo.


1000683462


Pia amewaomba Wakurugenzi wa OR- TAMISEMI na Wizara ya Afya kuangalia idadi ya Vijiji ambavyo havina Zahanati ili kuweza kuhakikisha vinapata vituo hivyo.


“Tukijipanga kwa muda wa miaka miwili tukapunguza semina na makongamano na tukapunguza mengine na mengine, tukapunguza kidogo kuboresha huku juu zaidi kwasababu huku tunaweza kwenda kwa pamoja nawahakikishia kwa kipindi cha miaka miwili hakuna Kijiji kitakosa Zahanati,”amesema.


Amesema hiyo itasaidia watakapokutana tena katika mkutano kama huo mwaka 2026 kuzungumza masula mengine kama kuweka watumishi, kuweka vifaa na kuboresha huduma zingine zinazopaswa kuwekwa.


Aidha amewaomba washiriki katika mkutano huo kuwasaidia wakurugenzi ambao bado wanaleta mgawanyiko katika kazi kuhakikisha suala hilo wanalimaliza na kuimarisha utendaji zaidi.


“Sekta ya Afya ni moja na kazi nyingi za afya zinaanzia katika ngazi ya msingi na dada yangu Dkt. Grace amesisitiza hapa hakuna huduma za afya bila msingi kwani huduma zote zinaanzia huko na wananchi wengi ndipo wanaanzia kabla ya kuja huku juu kupatiwa huduma,”amesema.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe amesema kuwa ili kufanikiwa katika sekta ya Afya ni lazima kuboresha kuanzia afya ya Msingi na ustawi wa Jamii


"Hakuna Afya bila Afya kuhakikisha eneo la Afya ya Msingi na ustawi wa Jamii lipo sawa,afya ya Msingi ndio Kila kitu ni muhimu kwani ndio Msingi wa sekta nzima ya afya," ameeleza Dkt. Magembe


1000683134


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Charles Mahela amesema kuwa kupitia mkutano huo mapendekezo mbalimbali yameweza kutolewa kupitia majadiliano yaliyofanyika ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa huduma za afya ya msingi.


“Mapendekezo hayo ni pamoja na kuongeza bajeti za afya za mifumo ya bima na jambo hili limesisitizwa kwa ukubwa na wakashauri vyanzo mbalimbali viweze kutumika ikiwemo kuwashirikisha wadau kama Wizara ya Fedha,”amesema.


Amesema pendekezo lingine lililotolewa ni kwa wadau pamoja na Serikali ni kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya afya ya msingi kwenye rasilimali watu na vifaa ili kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma bora.

IMG-20240328-WA0046
IMG-20240328-WA0045
IMG-20240328-WA0039
IMG-20240328-WA0036
IMG-20240328-WA0023
IMG-20240328-WA0021
IMG-20240328-WA0025
IMG-20240328-WA0026
IMG-20240328-WA0024
IMG-20240328-WA0018
IMG-20240328-WA0015
Share To:

Post A Comment: