Mkuu wa Mkoa wa Njombe Athony Mtaka amekabidhi mpango mkakati  kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga na Waziri wa Katiba na sheria Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Mpango mkakati huo wa miaka saba umekabidhiwa pia kwa viongozi wa dini , viongozi wa kimila pamoja na makundi mengine ili kila mmoja aweze kutambua anachotakiwa kutekeleza kwenye kampeni ya kuhamasisha lishe bora ili kuongeza kasi ya kupunguza udumavu Mkoani Njombe.

Kampeni ya Lishe ya Mwanao Mafanikio yake iliyozinduliwa Desemba 22,2023 ni kampeni endelevu ambayo inafadhiliwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo UNICEF na USAID kupitia mradi wa lishe mtambuka

Share To:

Post A Comment: