Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kushirikiana na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo kuandaa mfumo data utakaowezesha kutambua idadi ya waajiri nchini ili kuwapatia elimu ya pamoja ya kutatua migogoro ya kikazi.

Mhandisi Luhemeja ametoa agizo hilo Januari 06, 2024 Mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza na watumishi wa CMA katika kikao kazi cha tathmini ya utendaji kazi na mafunzo.

Aidha,Mhandisi Luhemeja ameitaka Tume ya usuluhishi na uamuzi kuongeza nguvu katika kutoa elimu kuhusu migogoro ya kikazi pamoja na kufafanua sheria zinazohusu kazi ili kusaidia waajiri na waajiriwa badala ya kukazana kupunguza idadi ya migogoro ndani ya Tume.

Ameongeza kuwa,migogoro mingine ya kkikazi inatokana na waajiri na wajiriwa kushindwa kuta mbua sheria za kazi huku wengine wakishindwa kuelewa na kupelekea migogoro baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Vilevile, Luhemeja amewasisitiza watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kuzingatia namna bora ya ufanyaji kazi kabla ya kudai maslahi yao amewataka waweze kuja na njia bora ya ni namna gani wanaweza kuboresha utendaji kazi wao.

Hata hivyo Mhandisi Luhemeja,ambaye ni mgeni rasmi katika kikao cha tathmini ya mafunzio na utendaji kazi wa Tume ikiwa ni siku ya mwisho yaKikao hiko, kilichofanyika mkoani Morogoro kuanzia Januari 04-06,2024 na kufunguliwa na Wazziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,Prof.Joyce Ndalichako.

Share To:

Post A Comment: