MKOA wa Kilimanjaro umepokea jumla ya magari 15 katika Sekta ya Afya kati ya hayo magari 10 ni ya kubebea wagonjwa (Ambulance), na magari 5 ni kwa ajili ya utawala ambayo yatatumika kwenye huduma za usimamizi shirikishi na usabazaji chanjo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ambapo alisema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya mapinduzi makubwa na uwekezaji katika miradi ya Maendeleo hususani sekta ya Afya.

Babu alisema kuwa, lengo la kuborsha sekta ya afya ni kuhakikisha Makundi yote kwenye jamii yanapata huduma za afya bora na zenye viwango vinavyotakiwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025.

“Magari haya ymepatikana kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya bora na zenye viwango hivyo  magari haya yatumike kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo” alisema Babu.

Share To:

Post A Comment: