Na Shushu Joel,Bukombe

MBUNGE wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt Dotto Biteko amefanikiwa kuzimaliza kambi za upinzani katika jimbo hilo pasipo kutumia nguvu ya aina yeyote ile bali ni kuwaletea maendeleo wananchi kwa kasi kubwa na ya ajabu ambayo haijawai kutokea kwenye jimbo hilo.

Wakizungumza na Mtandao huu wananchi wa wilaya ya Buseko walibainisha kuwa tangu jimbo hilo kuchukuliwa na Dkt Biteko kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali za kimaendeleo kama vile elimu,Afya, Umeme, Maji na miundombinu.

Tabu Ng’hwani (64) alisema kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto nyingi sana za maendeleo kwa wananchi lakini tangu Dkt Biteko aweze kuwa mwakilishi wa wana Bukombe jimbo limekuwa na neema kubwa za kimaendeleo.

Aliongeza kuwa kutokana na neema hiyo ya maendeleo katika jimbo la Bukombe tunampongeza sana kiongozi wetu wa jimbo ambaye amekuwa mwenye uchungu na maendeleo ya wananchi jambo ambalo linazidi kutupeleka katika ramani ya maendeleo.

Aidha amewakumbusha wananchi kuendeleo kumuunga mkono mbunge wetu Dkt Biteko kwa kumpatia heshima kubwa ya kumpatia ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwapigia kura viongozi wa CCM.

Naye Bi’ Sophia Shilinde amempongeza mbunge kwa kuwatua ndoo kichwani wanawake wa jimbo la Bukombe ambao kipindi kirefu walikuwa wakipambana na changamoto ya maji jambo ambalo lilikuwa ni kero kubwa kwa jamii.

Aidha amemsifu kwa ufanisi wa uwepo wa huduma za Afya katika kila kata jambo ambalo limechangia kupatikana kwa huduma bora kwa wanawake pindi wanapokwenda kupata huduma za uzazi.

Share To:

Post A Comment: