Na. Mario Mgimba 

Mkoa wa Njombe umepanga kuhakikisha maeneo yote ya uwekezaji na maeneo ya uzalishaji yanafikika kwa kuwa na miundombinu bora ikiwemo barabara maji na umeme. 

Akizungumza Mkuu wa Mkoa Njombe Mhe Anthony Mtaka katika Mkutano wa Jukwaa la Wadau wa Parachichi Uliofanyika Mjini Njombe amesema Serikali imejipanga kuhakikisha maeneo yote ambayo kunauzalishaji mkubwa kwenye kilimo kunapelekwa miundombinu yote ambayo inatakiwa kwa mkulima ili kukuza Uchumi katika Mkoa wa Njombe na kuwavutia wawekezaji kutoka nje ya Mkoa. 

Aidha Mhe Mtaka amewaonya wazalishaji wa miche ya zao la parachichi kuhakikisha wanazalisha miche ya parachichi yenye ubora na kiwango ili kuleta ushindani kwenye soko la kimataifa. 

“Tunatamani kuona zao la parachichi linalindwa kwa Mkoa wetu wa Njombe tuhakikishe kila mzalishaji wa zao la parachichi anazalisha kwa kiwango ambacho kina kidhi matakwa ya kitaifa na kimataifa kwa lengo la kuwa wazalishaji bora wa zao hilo Afrika na duniani”

Pia Mhe Mtaka amewaonya wakulima na wanunuzi wote wa zao la parachichi ambao watanunua parachichi ambazo hazijakoma kuchukuliwa hatua kwa pande zote mbili (muuzaji na munuaji) ,ambaye hata zingatia maagizo ambayo yametolewa kutoka ofisi ya kilimo ya Mkuu wa Mkoa  Njombe  na kwa wale ambao maeneo yao parachichi zinawahi kukomaa watapewa kibali rasmi  na watavuna kwa tarehe ambayo ofisi ya kilimo itakuwa imewapa ili kuepusha matapeli na watu ambao wana nia ovu ya kuharibu zao hilo .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wadau wa Mnyororo wa Parachichi Rebecca Hepelwa amesema Mkoa wa Njombe pekee unatarajia kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 38 kwa mwaka 2024 kupitia kilimo cha zao la Parachichi huku akiomba zao la parachichi kulindwa .

Sesilia Mloso Mkaguzi wa Afya ya Mimea Nchini amesema Serikali tayari imeweka mikakati ya kujenga maabara ya kuchakata viuatilifu katika zao la parachichi  Mkoani  Njombe na tayari bajeti kwa mwaka wa fedha 2024 hadi 25 ishatengwa kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima wa parachichi kutatua changamoto  katika zao hilo.

Share To:

Post A Comment: