Na Pamela Mollel,Arusha 

Viongozi wa Mila wa jamii ya wafugaji kutoka  tarafa tatu za wilaya  ya longido  Mkoani Arusha wameanza kuchukua hatua  za kuyatambua  na kuyalinda  maeneo yote  yaliotengwa  kwaajili ya nyanda za malisho ya mifugo

Hatua hiyo imekuja kipindi ambacho mvua  zinazoendelea kunyesha hali itakayosaidia  kukabiliana na ukosefu wa malisho wakati wa kiangazi

Wakizungumza wakati wilipokutana Viongozi wa mila kujadili  njia  bora  za kusimamia nyanda  hizo na kushughulikia changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi

Kiongozi wa mila Saron Kayongo kutoka longodo anasema wanaamini majadililiano hayo na wadau wahifadhi itasadia kwa kiwango kikubwa kulinda maeneo yaliyohifadhiwa ya nyanda za malisho

Afisa uhifadhi jamii na mazingira kutoka shirika la watu na wanyamapori TPW linalowajengea wafugaji uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi bwana  Kirerenjo Medukenya  anasema sababu za kukutanisha kundi hilo kwaajili ya kutoe elimu na mafunzo kwa Viongozi hao wa mila ili kutambua faidia ya kuhifadhi nyanda za malisho

Kwa upande wake Afisa mazingira  kutoka ofisi ya  Rais  Tamisemi Theodori Mlokosi anasema a kikao hicho kina manufaa makubwa kwa jamii kwani kitasaidia kuondosha migogoro ya wakulima na wafugaji

Wilaya ya longido ambayo aslilima kubwa ya wakazi wake ni wafugaji imekua ikikabiliwa na ukame wa muda mrefu unaoathiri malisho na wakati mwingine baadhi kulazimika kuhama makazi yao kwa ajili ya kunusuru mifugo yao.

Share To:

Post A Comment: