Na John Walter-Manyara
Sheikh wa mkoa wa Manyara Alhaj Sheikh Muhamad Khamis Kadidi kwa niaba ya Waislamu mkoani humo ametoa pole kwa wahanga wa Mafuriko wilaya ya Hanang' akiwataka kuwa watulivu na Subra katika kipindi hiki kigumu.

Aidha Sheikh wa Mkoa amewaagiza Viongozi wa Baraza kuanzia Mkoa, Wilaya , Kata, Misikiti na Jumuiya zote za Baraza kwa maana ya Jumuiya ya Vijana (JUVIKIBA) na Jumuiya ya Kina mama (JUWAKITA) kutoa Msaada kwa wahanga wote na Misikiti na majengo yote ya Baraza kutumika katika kutoa Msaada katika kipindi hichi.

Sheik Kadidi anawaombea Marehemu wote Allah aziweke Roho zao Mahala pema pamoja na kuwaombea majeruhi wote Allah awaponye haraka na kuwarejesha kwenye Shughuli zao za kawaida.
Share To:

Post A Comment: