Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ina mchango mkubwa sana katika sekta ya uhifadhi wa malisili na uboreshaji wa biashara ya utalii nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dunstan Kitandula  (Mb) wakati akizungumza na Mwenyekiti  wa Bodi na Menejimenti ya TAWIRI, Dkt.Kitundula alipotembelea ofisi za Makao Makuu ya Taasisi  ya Utafiti Wa Wanyamapori Tanzania(TAWIRI)  zilizopo Njiro, Jijini Arusha. 

Mhe. Kitandula alisema kuwa , tafiti za TAWIRI zinamchango mkubwa katika  sekta ya uhifadhi  na utalii nchini, ambapo  amewapongeza wataalamu  wa TAWIRI  kwa umahiri   na ubobevu, ambao umewaleta  wadau kutoka nchi mbalimbali  kuja kupata uzoefu kama vile sensa za wanyamapori.

"niwapongeze kwa umahiri wenu, kwani mnashiriki kukuza utalii kupitia  zao jipya la utalii wa utafiti " amepongeza Dkt. Kitandula.

Mwenyekiti  wa  Bodi  ya  wakurugenzi  TAWIRI, Dkt.David  Manyanza  amesema  bodi hiyo na wataalam kupitia mpango mkakati utakaohuishwa imeandaa vipaumbele vitakavyoongeza wigo wa  Taasisi  hiyo  kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kisayansi  kwa wakati ili kuimarisha uhifadhi na kukuza utalii nchini.

Awali,akitoa taarifa, Mkurugenzi  Mkuu  wa TAWIRI Dkt. Eblate  Ernest Mjingo  amesema  mbali na taasisi  hiyo kuwa na wataalam mahiri,   inatumia teknolojia  za kisasa katika tafiti ikiwa ni matumizi ya visukuma  mawimbi kuwafuatilia wanyamapori,  matumizi ya akili mnemba (artificial intelligence) kufanya sensa ya  wanyama.

Share To:

Post A Comment: