Na John Walter-Manyara

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amesema Watu 17 wamefariki dunia katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara kufuatia mafuriko yaliyoambatana na mawe makubwa na miti kuingia katika makazi ya Watu.

Mayanja amesema mvua hizo zilianza tangu Jana lakini maji yakawa yanaporomoka kutoka Mlima Hanang yakiwa na mawe na miti kuja katika Mji wa Katesh yakiwa na nguvu na kuingia kwenye makazi ya watu.

"Mpaka sasa tumepata vifo vya Watu 17 pamoja na majeruhi ambapo maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Tumaini lakini pia uharibifu wa miundombinu ya barabara kati ya Sindiga na Babati yamesimama kwa muda ila TANROADs na TARURA wapo hapa kuhakikisha mawasiliano yanarejea”

“Pia niwaombe Wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati jitihada za uokoaji zikiendelea”

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Tumaini iliyopo Katesh.
Share To:

Post A Comment: