Share

Diwani wa Kata ya Mirongo Hamidu Said akiwa ameshikilia fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Geradi Robert mwandishi wa habari aliejitokeza kuchukua fomu 

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Mwanza akiwemo mwandishi wa habari wamejitokeza kuchua fomu ya uenyekiti wa CCM Mkoani humo huku kila mmoja akieleza namna atakavyoitumikia nafasi hiyo.

Wakizungumza leo Novemba 15, 2023 na Fullshangwe Blog kwa nyakati tofauti wamesema wamechukua fomu ya uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza kutokana na nafasi hiyo kuachwa wazi na Mwenyekiti aliyekuwepo Sixbert Jichabu baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Masasi Mkoani Mtwara.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Sengerema Michael Makoye ni miongoni mwa waliochukua fomu amesema sababu za kuwania nafasi hiyo ni kuwatumikia wananchi,kukiimarisha Chama na kuendeleza mazuri ambayo watangulizi wake walishayafanya.

Amesema kuchukua fomu na kuijaza ni hatua ya kuomba ridhaa kwenye mamlaka ya Chama ili kuja kufanyiwa uteuzi wa kwenda kuomba na kupigiwa kura.

Kwa upande wake Diwani Kata ya Mirongo Hamidu Said amesema anawania nafasi hiyo kwasababu anauwezo wa kukisimamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akieleza Mkoa wa Mwanza hali ya Kisasa ilipofikia inahitaji watu wenye maamuzi sahihi na asiyekuwa na makundi.

Naye Geradi Robert ambae ni mwandishi wa habari amesema ameona anafaa kushika nafasi hiyo kwani amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chama huku akiahidi kuwaunganisha wanachama na kuhakikisha uchaguzi Mkuu 2025 ushindi unapatikana kwa kishindo.
Share To:

Post A Comment: