NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imetoa Pikipiki tatu za magurudumu mawili kwa ofisi ndogo za vidakio vya maji vya Kilosa, Msowero na Tuliani, lengo kuongeza ufanisi wa kazi kwa maafisa vidakio na kuwafikia wateja kwa urahisi pamoja na kuimarisha uhifadhi wa vyanzo vya maji hasa kwa maeneo ambayo hayafikiki kwa gari.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi Pikipiki hizo Mratibu wa vidakio kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Mohamed Msingi amesema Wami/Ruvu imejidhatiti katika kutunza na kuhifadhi vya vya maji hivyo Pikipiki hizo zitasaidia kufika maeneo yote  ya vyanzo, kuimarisha uhifadhi na kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wao Maafisa vidakio vya maji waliopata Pikipiki hizo  wameushukuru uongozi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  kwa kuona umuhimu wa kununua usafiri ambao unafika maeneo yote hata yale  yenye changamoto ya miundombinu ya barabara hasa kwenye mashamba ya wakulima ambao ni wateja wao pia.

Pia wamesema zitasaidia kuongeza mapato kwa kuwafikia wateja wapya na wazamani  ambao awali walikuwa hawezi kuwafikia kwa urahisi hivyo walikuwa wanapoteza  mapato.

“Pikipiki zitarahisisha sana utendaji kazi wetu kwani awali tulikuwa hatuwezi kuwafikia wateja wetu wote kwa urahisa hasa walima ambao wapo mashani, tulikuwa tunashindwa kuwafikia kutokana na changamoto ya usafiri, gari haliwezi kufika maeneo yote”. Alisema Afisa Kidakio Kilosa Christine Kipondya

Share To:

Post A Comment: