Na. Asila Twaha, Iringa


Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya TAMISEMI imeendelea kuonesha ubabe kwenye Michezo ya SHIMIWI yanayoendelea Mkoani Iringa.

Hayo yamejidhihirisha kwa timu hiyo kukosa mpinzani tangia mechi zinaanza kwa kucheza na kuzifunga RAS Kagera, Mashtaka na Wizara ya Mambo ya Nje.

Mechi iliyochezwa leo  Oktoba 2, 2023 katika viwanja vya Mkwawa timu ya TAMISEMI ilionesha uwezo mkubwa, umahiri na aina yake ya uvutaji na kufanikiwa kuivuta timu pinzani ya Mambo ya Nje kwa pointi 2-0.

Kocha wa timu hiyo Chediel Masinga amesema mwendo wao ndio uleule wa mazoezi kwa wachezaji wake sababu hakuna miujiza katika mchezo bali ni umoja,ushirikiano,heshima na mazoezi.

Ameongezea kwa kusema  michezo ya SHIMIWI inawapa nafasi na kuwakumbusha watumishi kuendelea kufanya mazoezi hata wanaporudi katika vituo vyao vya kazi amesema inasaidia panapokuwa na mashindano wanakuwa na utayari kama walivyokua watumishi wa timu ya kamba TAMISEMI.

Naye kapteni wa timu ya wanawake kuvuta kamba Saida Marijani ameushukuru uongozi wa  Wizara kwa kuwasapoti kila siku kuwajulia hali na maendeleo ya michezo amesema watajitahidi kuendelea kufanya vizuri ili kupata ushindi.

Share To:

Post A Comment: