Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella amefungua Kikao cha Uzinduzi wa utekelezaji wa Programu endelevu ya Maji na Usafi wa mazingira vijijini kwa kutumia utaratibu wa malipo kwa matokeo(Program for Results-PforR) mkoani Arusha.

 

Akifungua kikao hicho mkuu wa mkoa amesema kuwa ni jambo kubwa na lakiistoria la kuzindua Progrmu hiyo ambapo kwa mkoa wa arusha kwa hapo awali haukuwepo katika program hii ya PforR nakusababisha changamoto kubwa kwasababu katika progamu hii kuna fursa kubwa sana yakupata kupata tiba ya changamoto kubwa yam aji kutokana na mkoa huu kuwa na takribani ya asilimia 70 ya maeneo kame kwa kipindi kirefu cha mwaka.

 

“Shughuli kubwa ya wananchi wengi ni  ufugaji na kilimo ambacho kinategemea sana upatikanaji wa maji ya uhakika kwa Maisha yao kama binadamu lakini hata kwa mifugo na shughuli za kilimo Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kuamua na Arusha kuwa sehemu ya Programu hii ni jambo kubwa sana la kumshukuru”.alisema

 

 

Kwasababu ilituweze kutoka tulipo tunatakiwa kuwa na nguvu ya pamoja na uelewa katika ufuatiliaji wa ajendaa hii nyeti ya nchi wetu  maana  ilani ya chama cha mapinduzi inatueleza ifikapo 2025 lazima maji safi na salama  yapatikane kwa Zaidi ya  asilimia 85 kijijini na mijini kwa Zaidi ya asilimi 95 niwaombe viongozi wa chama ilani haishii tu kwenye utekelezaji wake tushikamane na kushirikiana kwa Pamoja kwenye usimamizi wa miradi.

 

“Kwakushirikiana na wakuu wa wilaya wakurugenzi na mameneja wetu chama na viongozi wote twende kwenye ngazi za vijiji tuwashirikisheke na tufatilie tusaidie kusukuma ajenda hii kwasababu Rais wa Tnzania ameshafanya kipande chake na sasa tumepewa fedha hizi bilioni 4.8 tukiendelea kufanya kazi tunauwezo wakupata hata bilioni 9 kwa kuongeza ufanisi ambapo mpaka mwaka  kwa ufuatiliaji na ufaninisi tuanze kwenye  ngazi ya kijiji na mitaa tuhakikishe tunasukuma jambo hili kwakuendelea kufanya kazi maana tunauezo na ufanisi ambao mpaka mwaka ujao tunaeza kufikia bilioni.20”.alisema

 

Naye meneja wa RUWASA Mkoa wa Arusha Bwana Joseph Emanuell Makaidi ,amesema kuwa program hii ya PforR ni mbinu mkakati ya utekelezaji wa dira ya 2025 serikali mnamo mwaka 2006 iliaanzisha mpango wa maendeleo ya usambazaji maji na usafi wa mazingira Tanzania ukiwa na lengo la kuiwezesha serikali kwa ujumla kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na dira ya Taifa.

 

“Mpango huu toka wakati huo umeshapitia awamu tatu Serikali ilifanikiwa katika awamu ya kwanza ya mpango huu kupata ufadhili kutoka benki ya dunua ambapo walitoa dola milioni 30,kama mkakati serikali ilianza na maeneo ambayo yalikua na hali duni sana ya upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira Pamoja na watu binafsi ambapo serikali ilitekeleza pragramu hii kwa mikoa 17 ilitekeleza kwa awamu ya kwanza kwa miaka miwili na mikoa mingine 8 kuongezwa baada ya mikioa mingine kufanya vizuri sana”.alisema

 

Hali ya usafi wa mazingira imeboreka hali ya udumavu imepungua ni vyema shughuli zozote kubwa tuzifanyane kwa Pamoja ilikuweza kufikia malengo kwa kusaidiana na tunakwenda kutekeleza program hii tukiwa na vigezo na tunategemea kuvuna Zaidi kama tukifanya kazi kwa ufanisi.

 

“katika mkoa wa Arusha kila wilaya imepatiwa shilingi milioni 961 kwaajili ya kutekeleza miradi ya miundo mbinu na uendelevu wa miradi na kuunda vyombo vya kusimamia huduma za maji katika eneo la maji tutaendakutekeleza miradi ambayo itatoa matokeo kwa vigezo vilivyowekwa ili kupata matokeo makubwa”.

 

 

Fedha ambazo tumeletewaa ziweze kufanya kazi iliyokusudiwaa nakuahidi mkoa wa Arusha kutokumuaangusha Rais maana fedha hizi n kama mbegu inatakiwa izaee....tumeaminiwa kuwatumikia wananchi...mkuu wa wilya ya karatu

 

Naye mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Tanzania Mhandisi Ruth Koya,  amesema kuwa program hii ya  Maji na Usafi wa mazingira vijijini kwa kutumia utaratibu wa malipo kwa matokeo(Program for Results-PforR) itawasaidia sana RUWASA kuhakikisha wanafanikisha adhima ya serikali ya awamu ya sita ya kumtua mama ndoo kichwani.

 

Hata hivyo Mbunge viti maalumu mkoa wa Arusha  Zaitun Swai kwaniaba ya wabunge wa mkoa huo amesema kuwa program hii kwa upande wa akina mama itawasaidia sana kwasababu lengo kuu ni kumtua mama ndoo kichwani kwasababu kwa kiasi kikubwa wanawake wanateseka sana na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa hiyo kwakupewa hizo milioni 961 zitawasaidia wananchi wa mkoa huo na kuwatua akina mama ndoo kichwani .


Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Arumeru Noel Emanuel,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama kwa uaminifu “Sisi kama Chama tunatambua wajibu wetu ni Kusimamia Ilani na tutawapa ushirikiano asilimia 100 ilikuweza kufikia malengo yetu kama tulivyowaahidi wananchi“.alisemaShare To:

Post A Comment: