Na Prisca Libaga Arusha
Wakazi wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi viwanjani ili kuzisaidia na kuzipa hamasa Timu zao kuweza kupanda ligi Kuu msimu ujao.
Aidha baada ya Msimamo wa Nbc Championship kukamilika Kwa mzungo wa Nne Kwa Kila timu,umekuwa mwanzo mzuri Kwa timu kutoka Arusha yaani Mbuni fc na Tma stars football kuwa miongo mwa timu ambazo hazijapoteza mchezo Hadi sasa.
Akizungumza Jijini Arusha Katibu Tawala Mkoa huo Missaile Mussa amewataka wakazi wa Mkoa huo kuendelea kujitokeza viwanjani na kutokaa kinyonge kwani timu zetu zipo vizuri ni muda wa kuzisapoti ili kurudisha hadhi ya Mkoa wetu.
Kwa Mujibu wa Katibu Tawala Mkoani hapa hadi Sasa Mbuni wamepoteza alama 2 kati ya 12 ni kitu kizuri pia kuchukua alama 6 ugenini wakati huo wana mechi 3 nyumbani.
Ifike Mahali Wanaarusha tujenge Umoja mshikamano ili kuwezesha Timu zetu msimu huu kupanda Ligi Kuu kwa kujitokeza viwanjani kuzipa morali ili wageni kuiona Sheikh Amri Abeid ni sehemu chungu kwa ajili ya kukusanya alama zote katika mechi za nyumbani kutokana na hamasa yetu.
Vile vile Chama la TMA Stars Ikiwa ni msimu wao wa kwanza kabisa Champion ship hawajaja kinyonge Hawa ni washindani halisi haswa katika alama 12 wameondoka na alama 8 wakipoteza alama 4 pasina kufungwa mechi ni mwanzo mzuri sana kama tutawapa morali.
"Kitu Muhimu sasa kuna mechi 3 nyumbani hizi ni lazima tupate alama 9 ni muhimu katika uwanja wa nyumbani Tena kwa kufunga Magoli mengi tukishikamana na kujenga Umoja hakika tutaondoa unyonge wa michezo ya ligi Kuu kuiona kwenye runinga"
Wanaarusha tunasema tunaitaka Ligi kuu Sasa twendeni viwanjani kwa wingi kuvishangilia vilabu vyetu vyote viwili kwani kama Mkoa tumejipanga kurudisha hadhi yetu.
Next ni Mbuni 🆚 TMA Stars octoba 7 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid hii ni Derby.
Post A Comment: