Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Wa Chipukizi wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha Wamchagua Ndugu Nasma Ally Karanjay Kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi  Wilaya ya Ngorongoro kwa Kura 100 dhidi ya wagombea wenzake wanne.

Akizungumza mara baada  ya uchaguzi huo Nasma amesema nashukuruni sana kwa kunichagua namimi nitakuwa kiongozi wa chipukizi wote na sio wa kundi lolote,nanyie vijana wenzangu tunaochipukia tuendelee kukupenda Chama cha Mapinduzi na kukilinda.

Kwa upande msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Katibu wa Uvccm Wilaya ya Ngorongoro Lobikiek Mollel amesema kuwa wanawapongeza sana chipukizi kwakufanya uchaguzi kwa amani pia anawapongeza sana wagombea kwani wakati kila mgombea mmoja alipokuwa anajinadi alikuwa anaongelea kukijenga chama na kuyaenzi yale yote yanayofanywa na Rais samia 
"Nawapongeza chipukizi wangu wa Ngorongoro kwakuwa vijana wamejitambua na wamejua hatukua tunashidwa uchaguzi wowote bali makundi ndio yanawamaliza na wameahidi kuvunja makundi yao ,naunajua amna uchaguzi bila makundi bali makundi hayo yanatakiwa yavunjwe tu mara baada ya uchaguzi kuisha na tumeona hapa vijana wameyavunja mapema makundi hayo na wametangaza hatharani hivyo napenda sana kuwapongeza"alisema

Share To:

Post A Comment: