Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nachingwea Rashid Likongo akiwafunda wanafunzi wa shule ya sekondari Nambambo wilayani Nachingwea


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MWENYEKITI wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nachingwea amewataka wanafunzi wa kidato Cha pili na kidato cha nne katika shule ya sekondari Nambambo kuongeza umakini kwenye mitihani ya Taifa wanayoenda kuifanya hivi karibuni.

Akitoa nasaa hizo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nachingwea Rashid Likongo alisema wanapaswa kutuliza akiri na kufanya mtihani kwa umakini mkubwa ili kufanya vizuri kwenye matokeo yao kwa faida yao 

Likongo alisema kuwa maisha bila elimu ni magumu hivyo wanapaswa kufanya vizuri ili kupiga hatua kwenye kila mtihani ambao wanakabiliana nao kwa faida ya Taifa na yeye binafsi.

Alisema kuwa elimu ndio msingi bora wa maisha ya kila mwananchi katika kukuza uchumi na maendeleo ya Taifa na familia zao hivyo waachane za Mila potofu na wazingatie masomo yao 

Likongo aliwataka wanafunzi hao kuacha kuigia tabia za mitaani zisizo na maadili bora ambazo zimekuwa zikiharibu maisha ya wanafunzi wengi na kutumbukia katika ulevi wa vilevi mbalimbali.

Alimazia kwa kuwatakiwa mtihani mwema kwa kufanya vizuri na wote kufaulu Kwa alama A na B ambazo zitawapa sifa ya kuendelea na hatua nyingine za kimasomo.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: