Na John Walter-Mbulu

Mwenge wa uhuru umezindua daraja jipya la Barazani katika barabara ya MAGHANG -Maghang-Endanachan-Endamilay uliojengwa na Serikali kupitia wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Kwa gharama ya shilingi milioni 249. 98. 

Daraja hilo linahudumia Wananchi wa vijijini vitatu vya Barazani,Maghang na Endanachan  ni utekelezaji wa ahadi ya serikali ya chama cha Mapinduzi -CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye lengo lake ni kumtua mama ndoo kichwani. 

Mradi huo ni sehemu ya jumla ya miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni  1.8 iliyopitiwa na Mwenge wa uhuru Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 inasema “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”Share To:

Post A Comment: