Na Mwandishi Wetu


MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango ameeleza kwamba Serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda vya dawa lakini kwa kuwa uamuzi huo ni wa Rais Dk. Samia Suluhi Hassan hakuna atakayefanikiwa kuvikwamisha na kusisitiza viwanda hivyo vitajengwa.

Akizungumza jana Mkoani Njombe wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha mipira ya mikono (Gloves) kinachosimamiwa na Bohari ya Dawa ( MSD), Makamu wa Rais Dk. Mpango amesema kwa sasa Serikali inaagiza dawa kwa asilmia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 kutoka nje ya nchi.

Amefafanua hali inayosababisha uhaba wa vifaa na gharama kubwa za uagizaji wa vifaa vya afya hivyo ni lazima kuchukua maamuzi magumu huku akieleza lazima vijengwe viwanda vya dawa na vifaa tiba japo inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda hivyo vya dawa.

Amesisitiza Rais Dk. Samia ameamua hivyo viwanda hivyo vitajengwa kwa gharama yeyote kwa kuwa nchi ina uhaba wa dawa na vifaa tiba .“Bidhaa hizo zinaagizwa kutoka nje dawa zinaagizwa kwa asilimia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90.

"Tumeamua kuipatia MSD majukumu manne ambayo ni uzalisha, ununuzi, utunzaji niwahakikishie viwanda hivi vitajengwa.Ujenzi wa viwanda hivi umelenga kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kupunguza matumizi fedha za kigeni, uhaba wa dawa, gharama kubwa kuagiza bidhaa hizo na kutoa ajira,”amesema.

Aidha Dk.Mpango amesifu hatua ya utekelezajiwa mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 90 kutoka asilimia 30 ambapo Rais Samia alikuta ujenzi ambao umekamilishwa na wataalamu wa ndani kwa kushirikisha Mamlaka husika.

“Uwepo wa kiwanda hiki ni muhimu sana kwa ajili ya mahitaji ya ndani na nje ya nchi wakati wa Corona tulihangaika sana matumizi ya gloves ni makubwa kiwanda hiki ni mkombozi hivyo lengo la Rais Dk. Samia lazima lifikiwe,”amesema.

Dk. Mpango amesema, wapo katika mkakati wa kuiongezea mtaji MSD ili kujenga viwanda na maghala na kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba."Nataka uzalishaji wa kiwanda uanze mara moja Januari mosi mwaka 2024 na kiwanda hiki hakitoki hapa kitabaki...

"Kitazalisha niwaagize MSD ongezeni uzalishaji mwingine wa maji tiba na vitendanishi na kampuni Tanzu ya MSD zingatieni misingi ya kibiashara na watumishi zingatieni uzalendo.

“Pia niliagiza na nasisitiza tena watumishi wote wafanyiwe veting wale wanaotumiwa na wafanyabiashara kwa maslahi ya mifukoni mwao tuchukue hatua, ukipewa dhamana katika taasisi za umma zingatia maadili,”amesema

Dk. Mpango alieleza kuwa, ameteta na Rais Dk. Samia akiwa katika tukio hilo na kuagiza Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (TAMISEMI), kupitia Wakala wa Barabara Vijijini wafanye tathimini ya ujenzi wa barabara ya kwenda katika kiwanda hicho ambayo inahitaji bilioni 1.4 ili ijengwe kwa kiwango cha lami.

“Hiyo ndio salamu ya Rais mimenong’ona naye hapa hapa kasema hashindwi kujenga barabara hii hivyo nawapa wiki mbili TAMISEMI malizeni tathimini ujenzi uanze,”mesema.

Pia ameiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha zilizotengwa kupunguza deni la MSD zitolewe haraka iwezekanavyo ili wasiendelee kulia lia.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Molel amesema Wizara inatambua mapinduzi makubwa yanayofanywa na Rais Dk. Samia na serikali yake katika kuleta mapinduzi sekta ya viwanda hususani vya dawa.

Kutokana na hali hiyo aliahidi wizara itahakikisha hakuna kinachokwama na kiwanda hicho kitaanza uzalishaji mbali na vita kubwa iliyopo.

“Tutatoka salama Waziri Ummy atahakikisha kiwanda hiki kinazalisha, tunajua vita ni kubwa changamoto ni nyingi, tutashirikiana na bunge na taasisi nyingine tutakwenda,”alisema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema kiwanda hicho kimeanza uzalishaji wa awali na kinatararajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Amesisitiza kiwanda hicho kitasaidia kukuza uchumi na ndani ya miaka minane kitarudisha faida ambapo kwa mwaka wa kwanza faida itakuwa ni zaidi ya bilioni moja na ajira 200 kwa moja kwa moja na za muda.

Ameongeza kiwanda cha mipira ya mikono (gloves) Idofi hadi kikamilike kitagharimu sh. bilioni 22.5, baada ya kukamilika kwa ujenzi na ufungaji wa mitambo, kiwanda hiki kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mipira ya mikono 20,000 kwa saa sawa na jozi(pairs) 10,000 na hivyo kufanya uzalishaji wa takribani jozi 86,400,000 kwa mwaka.


Share To:

Post A Comment: