Na Heri Shaaban (Ilala )
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kivule Reuben Mduma, ameunga mkono Juhudi za Serikali kwa kuchangia tofali 1000 katika Harambe ya shule ya Msingi Misiti Wilayani Ilala katika mahafali ya darasa la Saba shuleni hapo.
Mwenyekiti Reuben Mduma. alichangia tofali hizo shuleni hapo jana ambapo alikuwa mgeni rasmi amechangia tofali hizo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa ukuta wa shule ambapo katika shule hiyo kuna changamoto wananchi wanakatisha kutokana na shule hiyo aijajengewa ukuta .
"Tunaunga mkono Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan. katika sekta ya elimu Ili kuiwezesha Mazingira bora ya elimu shuleni leo tumechangia tofali 1000 za kujenga ukuta kwa ajili ya kuimalisha usalama "alisema Mduma .
Mduma alisema yeye ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM kata ya Kivule atashirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbali mbali ndani ya kata hiyo katika sekta ya Elimu .
Aidha Diwani wa kata ya Kivule Nyasika Getama alichangia tofali 100 katika shule hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kerezange Ismail Ibrahim tofali 100 na mgeni mwalikwa Mwenyekiti wa wazazi kata ya ILALA SABRY SHARIF alichangia tofali 200 katika kuunga mkono Serikali katika sekta ya Elimu
Wengine waliochangia ujenzi wa shule ya Msingi Misitu katika harambee katibu wa CCM wa Kata Kivule Aissack Kibiti ,Katibu wa jumuiya ya wazazi CCM Kivule Sabrina Magarati wao walitoa cement mifuko kumi .
Wakati huo huo Mwenyekiti Reuben Mduma alitoa zawadi kwa walimu 26 wa shule hiyo kila mmoja kitenge sehemu ya motisha na shuka kwa walimu wa kiume wanne kwa ajili ya kukuza taaluma shule hiyo ambayo kila mwaka inafanya vizuri matokeo ya Elimu Msingi ngazi ya Wilaya ,Mkoa mpaka matokeo ya Taifa .
Post A Comment: