Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano Kimataifa  Arusha (AICC) Ephraim Mafuru amesema kuwa kumekuwa na faida kwa kituo hicho kutokana na juhudi zilizifanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kufungua Diplomasia ya uchumi na kufanya kituo hicho kuwa  na mikutano mingi.


Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuonesha Uthubutu katika kuhakikisha Diplomasia ya Uchumi wa Tanzania inaimarika kupitia Diplomasia ya Mikutano ya Kimataifa, ambayo pia inatajwa kufungua nchi kupitia Sekta mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Mafuru ameyasema hayo   Jijini Dar Es Salaam ukiwa ni mwendelezo wa Vikao kazi baina ya Taasisi na Mashirika ya Umma Chini ya Uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema wageni wanapenda Tanzania kutokana na juhudi zilizoonyeshwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo ni kazi kwao kuendelea kukaribisha wageni na taasisi mbalimbali kufanya mikutano nchini.

Amesema kuwa mikutano hiyo ikifanyika nchini inaongeza fedha za ikiwemo dollar pamoja na kuchangia shughuli zingine kwa wageni kufanya huduma mbalimbali.

Mafuru amesema kuwa mpango wake ni kwa kila mfanyakazi katika taasisi hiyo wanakwenda kila mmoja kujipima na ambao hawatafikia malengo wataoandolewa ikiwa ni kutaka kukua katika sekta hiyo.


Amesema Tanzania katika kufanya mikutano imeshika nafasi ya Tano kutoka nafasi 18 ambapo hatua hiyo mafanikio kwao ni ndogo kwa kutaka kujenga majengo mengine ya kuchukua watu zaidi ya 5000 kwa wakati mmoja na michoro tayari.

"Wageni kutoka mataifa mbalimbali wanavutiwa kuja Tanzania kwa hilo ninamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya Kufungua nchi, Ninajua kuna Royal Tour, lakini amekuwa akishiriki mikutano mbalimbali kuitangaza nchi, hatua ambayo imesaidia Tanzania kuwa chaguo muhimu na Kuvutia mikutano mbalimbali ya Kimataifa" amesema Mafuru.

Mafuru amesema katika tafiti walizofanya wamejiridhisha kuwa Diplomasia ya Mikutano itaendelea kuwa nguzo ya Kuongeza fedha za Kigeni na Kuimarisha Uchumi pamoja na pato la taifa

Aidha amesema  katika kuendelea kuwa na mikutano hiyo kuna baadhi ya Taasisi za Serikali zimekuwa  hazilipi madeni na kutaka walipe ambapo hayo madeni yamefikia bilioni Saba (7)

Hata hivyo amesema kuwa licha kuwa vituo vya mikutano wana Nyumba ambapo wanakwenda kuboresha zaidi huku wakiwa na hospitali ambayo inatoa huduma kwa wananchi katika jiji la Arusha

Amesema baada ya kampeni kubwa ya kufungua mipaka ya nchi katika utoaji wa huduma katika vituo vya mikutano wamekuwa na asilimia 10 ya Market Share kwa Afrika  malengo yao ni kwenda mbali zaidi.


Share To:

Post A Comment: