Hayo yamesemwa na Mbunge  wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Msukuma ,wakati akizungumza na wananchi  Wilayani  Longido Mkoani Arusha, katika Tafrija ya kusimikwa uongozi wa Mila wa ukoo wa Mamasita (Alaigwanani) ,Mh Alais Mushao ambaye ni Diwani wa kata ya Mundarara.

Awali akizungumza kwa niaba ya Madiwani Mh Saimon Oltesoi Laizer , ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Amempongeza Diwani huyo kwa kuaminiwa na Ukoo huo wa MAMASITA Kuwa kiongozi wao na kuendelea kuonyesha Umoja alokuwa nayo kwenye Baraza la madiwani bila ubaguzi, na kumuomba Mgeni Rasmi katika Tafrija hiyo ambaye ni Mbunge Msukuma kuwa sauti ya wafugaji Bungeni.

" Mheshimiwa mgeni Rasmi kwanza Karibu Longido, Alais tuligombea wote kiti Cha mwenyekiti wa Halmashauri Mimi nikashinda lakini nikiri kuwa tumekuwa pamoja katika KAZI , ni mtu ambaye Hana ubaguzi na ana Upendo kwa watu wote niseme ukoo wa mamasita wamempata Alaigwanani mzuri, Mheshimiwa msukuma wewe umekuwa sauti ya Wafugaji Bungeni na Leo umefika hapa kama unasikiaga neno NATRON ndo hapa Sasa tunaomba uwe sauti kwetu kuhusu maeneo yetu ya Malisho yanayotakiwa na Serikali kutengwa kama mapori tengefu, sisi ni wamasai kuishi na wanyama ndio maisha yetu , Maisha ya mseto tumezoa , wewe ni mjumbe Halmashauri kuu taifa tunaomba kama itawezekana serikali kuliangalia hili" Mh Saimon Oltesoi

Kwa Upande wake Mbunge WA Jimbo Hilo ambaye pia ni Naibu waziri wa Madini Doctor Stephen Lemomo Kiruswa , Amesema tayari ameshazungumza na waziri wa Utalii, Ufugaji ili kuweza kuona namna ya kuwasaidia Wananchi waliopata Taharuki kuhusu barua iliyotolewa kwa ajili ajili ya kutenga mapori tengefu kwa Wilaya za kifugaji na kuahidi Mawaziri hao kufika katika Maeneo hayo .

Aidha kwa Upande wake Laigwanani Alais Mushao aliyesimikwa hii Leo , Amesema naye anaungana na wenzake kuomba Serikali kuangalia namna ya Kuwaangalia jamii hiyo ya kifugaji kuhusu Ardhi kwa ujumla , na kusema ukoo wa mamasita wajivunie kumchagua yeye kwani atawasaidia  kwa namna yeyote Ile, muda wowote ule na kujua muda wa Majukumu ya Serikali na Jamii iliyomchagua.

"Leo tupo hapa katika sherehe yangu ambayo jamii na ukoo wa mamasita wameona nafaa kuongezewa jukumu lingine la Ulaigwanani tofauti na kiti changu Cha Udiwani, Naahidi kuungana na viongozi wenzangu Malaigwanani kuwa wamoja katika majukumu ya kijamii, kamwe sitakuwa chanzo cha migogoro." Alais Mushao Alaigwanani

Baada ya kusikiliza salamu mbalimbali kutoka kwa viongozi WA Mila , Chama na Serikali Mbunge Msukuma alisimama na kuwapongeza Jamii hiyo Kuenzi na kuendeleza Mila na Desturi zao, na Kuwahidi jamii hiyo kuwa Atakuwa sauti Yao kweli kama ilivyokuwa ni Tabia yake bungeni.

" Mnajua Masai na Msukuma hatuna tofauti ni Bora mtu akalime kuliko kufuga , kufuga ni ngumu sana ni Zaidi ya Malezi manake Ng'ombe haongei, mbuzi haongei , unaweza kununua ndama wako mmoja ufuge Hadi wafikie watano ni kazi ngumu sana , Lakini mimi Naamini Serikali ya Mama yetu Samia Suluhu Hassan ni sikivu hakuna mtu wa kuondolewa kwenye Eneo lake , Mfugaji anahitaji eneo Pana kwa ajili ya kufuga ."

Wakati huohuo akiwa jukwaani Alimpigia Waziri wa Maliasili ,Mohamed Mchengerwa ambapo alisikika akisema hakuna mtu atakayeondolewa na tayari Serikali inafanya Tathmini  na Ameahidi kufika katika Wilaya hiyo na kusema Maeneo pekee yatakayotengwa kuwa mapori Tengefu ni Mapori ambayo hazina matumizi yeyote ya kibinadamu.

Ikumbukwe Katika Tafrija hiyo ya kusimikwa kwa Alaigwanani wa ukoo wa Mamasita mheshimiwa Alais Mushao ambaye ni Diwani wa kata ya Mundarara, viongozi na watu mbalimbali maarufu walihudhuriwa , Wakiwemo Viongozi wa Chama wilaya ya longido na nje ya longido , wafanyabiashara wa Madini wakiongozwa na Simba Noah, Mawakili , Watumishi wa Mungu, Viongozi wa Mila kutoka koo zote, pamoja na wananchi ndani na nje ya wilaya hiyo.

Share To:

Post A Comment: