Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Serikali inalenga kuinua uzalishaji wa zao la alizeti na kukuza kipato cha wakulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe.Suleiman Mwenda wakati wa Kongamano na Mafunzo ya wakulima wa zao la alizeti kwenye maonyesho  nanenane Kanda ya kati katika viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma. 


Kongamano hilo limelenga kuunga mkono na kutekeleza kwa vitendo Juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuinua na kuthamini mchango wa Kilimo katika Taifa letu. Mafunzo hayo amebebwa na kauli mbiu inayosema ”alizeti kwa afya bora na kipato.

”Tumeshuhudia Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe inayotilia mkazo wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya alizeti ili kupunguza uingizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi na hivyo kupunguza matumizi ya bidhaa za kigeni. Jitihada hizo ni pamoja na kutoa ruzuku za mbegu bora na alizeti na vitendea kazi kwa maafisa ugani “ameeleza Mwenda 


Hata hivyo, Mhe. Mwenda ametoa wito kwa wadau wa kilimo kupeana uzoefu kuhusu mafanikio, changamoto na mkakati ya kuongeza tija ya uzalishaji na masoko ya zao la alizeti kwani sekta ya kilimo na mifugo inachangia uchumi wa nchi kwa zaidi ya asilimia 75 na kwa wananchi wa Dodoma na Singida huku alizeti ikiwa ni zao kuu la biashara katika Mkoa hiyo miwili .


Mhe. Mwenda amezitaja moja ya sababu zinazokabili mnyororo mzima wa zao la alizeti na hivyo kulazimu kuendelea na uingizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi kuwataka wadau kutumia Kongamano hilo kuweka mikakati ya kuzipatia ufumbuzi, ambazo ni kiwango kidogo cha uzalishaji, mabadiliko ya tabia ya nchi na masoko ya alizeti yasiyo kuwa na mfumo rasmi.


 Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema amewataka wakulima wa Mikoa ya Singida na Dodoma kutumia fursa hiyo waliyoipata kufanya kilimo cha tija na kuacha kilimo cha mazoea kutokana na mafunzo waliyo yapata kuhakikisha wanafanya kwa vitendo kama ilivyo dhamira ya Serikali.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: