Na John Walter-Manyara

Mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Babati (SSP) Peter Ngolo, amewaonya wananchi wanaojichukulia sheria mkononi na badala yake wafike katika vyombo vinavyohusika kutoa taarifa.

Ametoa onyo hilo alipofika kata ya Ufana kutoa elimu Kwa wananchi juu ya umuhimu wa kushirikiana na Jeshi hilo ili kukomesha vitendo vya uhalifu na ukatili katika maeneo yao.

Kwenye kata hiyo mapema mwezi Januari mwaka huu Mwanaume mmoja katika kijiji cha Saydoda alimuua mkewe na kukimbia akiacha watoto Watano, mmoja akiwa bado ananyonya.

Ngolo amewataka wananchi wanapofika Kuripoti jambo kituo cha polisi wafike na Barua ya utambuzi Kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji au kata husika.

Aidha amewataka Wananchi wa kata ya Ufana kuanzisha vikundi vya polisi jamii kwa ajili ya ulinzi katika maeneo yao.

Pamoja na hayo ameowamba wananchi waache kufanya Biashara ya kuuza pombe majumbani na badala yake watenge maeneo kwa ajili  hiyo na muda wa mwisho iwe saa tano Usiku.

Share To:

Post A Comment: