Waziri  wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa amewataka Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)  kudhibiti ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya watu wachache ili kuiongezea Wizara mapato, kufikia Dola milioni sita ambayo ni sawa na shilingi trilion 14 ifikapo 2025. 


Mchengerwa ameyasema hayo alipotembelea banda la TFS kwenye maoneosho ya 30 ya wakulima nanenane Kanda Mashariki Mkoani Morogoro katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 

Amesema  kuwa wao kama wakala wanamiliki zaidi ya asilimia 52 ya ardhi ya misitu sawa na kilometa za mraba 430000 hivyo anategemea waongeze jitihada pamoja na kuhakikisha kile kinachovunwa ndicho kilicholipiwa.

"Pamoja na kwamba mnafanya kazi nzuri, pelekeni hizi salamu kwa Kamishna wa Uhifadhi TFS (CC), nataka muongeze udhibiti wa ubadhilifu, kile kinachoandikwa kwenye kibali kiwe ndicho kinachovunwa. Alisema Waziri Mchengerwa.

 Amesema hapo awali  kuna aina ya miti iliyokuwa imezuiliwa kuvunwa kwa muda mrefu, kwa sasa tayari Wizara imeshafanyia kazi suala hilo, hivyo amewataka watumishi wa TFS   kufanya kazi kwa bidii na kufuata Maadili ya utumishi wa Umma.

Aidha amesema anayetakiwa kupewa kibali cha kusafirisha mazao ya misitu hasa Mkaa ni yule mwenye usafiri wa Maguludumu matatu ( mataili) au manne na kuendelea na sio Pikipiki ( bodaboda) na kwamba hategemei kuona TFS inawakamata wasafirisha mkaa kwa Pikipiki barabarani.

Awali, Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS Mathew Ntilicha alisema kuwa wao kama wakala wanafanya uzalishaji wa Miche ya miti na kwamba baada ya kufanya utafiti wamegundua kuwepo kwa baadhi ya miti inayoweza kuwa mbadala wa miti ya asili katika matumizi.

 Aliitaja miti hivyo kuwa ni pamoja na mininga,mikongo na mpingo.


Share To:

Post A Comment: