Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan akiongea wakati wa kongamano la madini lililofanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi huku akielezea fursa mbalimbali zinazotokana na upatikanaji wa madini katika mkoa huo.


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan amesema Lindi utakuwa mkoa tajili Tanzania kutokana na uwepo wa madini ya Kila aina katika ardhi ya mkoa huo.


Akizungumza wakati wa kongamano la madini lililofanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi,Mbunge Maimuna Pathan alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Lindi wanatakiwa kuzitumia vilivyo fursa za uwepo wa madini katika ardhi ya mkoa huo ambao utakuza uchumi wa taifa zima.


Pathan alisema kuwa baada ya miaka mitano kila mtu anatakuwa anazungumzia utajiri wa madini uliopo katika katika mkoa wa Lindi tofauti na ilivyokuwa awali.


Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa zote zilizopo kwenye sekta ya madini ili kukuza uchumi wao na kupata maendeleo kutokana uwepo wa madini mbalimbali.


Pathan alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na utunzaji wa mazingira kwenye maeneo ambayo madini yanachimbwa 

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: