Na John Walter-Babati

Wananchi wa kata ya Himiti wilayani Babati mkoani Manyara wamemshukuru Paulina Gekul ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini kwa kuwasemea na kuwatetea na kufanikisha kata hiyo kupata miradi mingi ya Maendeleo ambapo awali haikuwepo.

Wazee wamesema kwa Makubwa aliyowafanyia hawana Cha kumpa Mbunge huyo ila watamuongezea miaka mingine tena ya kuongoza Jimbo la Babati Mjini.

Wananchi hao wamemshukuru kwa kumzawadia zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kumtia moyo kazi majukumu yake ya kuwatetea Wananchi Bungeni na hatimaye kufanikisha kukamilika ujenzi wa matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Himiti miradi ya barabara,miradi ya Afya pamoja na kuwajengea shule ya Sekondari na Wananchi kuamua kuiita Gekul Secondary school.

Baada ya kupokea Pongezi hizo Gekul amewashukuru Wananchi hao huku akiwahakikishia kuendelea kuwaletea Wananchi hao miradi mingine mingi ya Maendeleo katika Jimbo Hilo ilo Hadi kufikia 2025 ilani ya CCM iwe imekamilika.

Mbunge Gekul leo anahitimisha ziara yake katika Kata ya Himiti na Kufanya kutembelea miradi ya Jimbo Zima ndani ya Siku saba na kufanikiwa kukagua miradi ya Maendeleo ikiwemo ya Afya,Elimu na Ujenzi wa ofisi za Mitaa huku akiahidi kuongeza nguvu kazi kupitia mfuko wa Jimbo.

Share To:

Post A Comment: