Mbunge wa kilolo mkoani Iringa Justine Nyamoga akiongea wananchi wa Kijiji Cha Kising'a juu ya ujenzi wa shule ya msingi katika Kijiji hicho


Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Mh Justine Nyamoga ameleta neema kwa wanakijiji wa kisin’ga baada kuahidi kuanza ujenzi wa shule ya Msingi  Kising'a ili kunusuru watoto wanaotembea umbali mrefu kufuata elimu.


Nyamoga yupo kwenye ziara inayolenga kusikiliza kero za wananchi wake katika Jimbo la Kilolo.


 Amesema ujenzi wa shule hiyo utaanza mara moja ili ifikapo January mwakani,  wanafunzi waanze kusoma katika shule hiyo 


Hata hivyo Nyamoga amewataka wananchi wa Kising’a kushiriki katika ujenzi wa shule hiyo ili iende kwa haraka na wanafunzi waanze kusoma mapema


“Niwaombe wananchi katika ujenzi wa shule hii kutakuwa na ajira nyingi sana sio vizuri wanakijiji wa kijiji kingine kuja kushiriki hapa naomba katika ujenzi wa shule hii kutakuwa na ajira naomba wanakijiji wa kata hii ndo muwe kipaumbele katika kupata ajira “ amesema Nyamoga

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: