Mbunge wa Singida Mjini, Musa Sima akiangalia choo cha Walimu wa Shule ya Msingi Ititi ambacho kimefungwa na kusababisha walimu kukosa sehemu ya kujisaidia alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Julai 21, 2023 Kata ya Uhamaka na kujionea changamoto hiyo.

.......................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Singida Mjini, Musa Sima amewashukuru  wananchi wa Kata ya Uhamaka kwa usimamizi na ukamilishaji wa ujenzi wa shule bora ya Sekondari jambo ambalo limemuheshima pamoja na Rais Samia Suluhu Hassam ambaye alitoa zaidi ya Sh.Milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.

Sima alitoa shukurani hizo Julai 21, 2023 alipokuwa  akihutubia kwenye mkutano wa hadhara baada ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

"Tulikuwa na changamoto kubwa mbili za shule na umeme nilimuomba Mungu siku nikija kusimama tena katika viwanja hivi ziwe zimetekelezeka hama zinatekelezeka na leo ninapo simama hapa shule tayari imekamilika na wanafunzi wanasoma na ninyi ni mashahidi kwa jinsi kulivyokuwa na changamoto kubwa ya elimu vijana walivyokuwa wakitembea zaidi ya kilometa 17 kwenda Shule ya Sekondari ya Mandewa ambayo ilikuwa na wanafunzi wengi kuliko uwezo wake," alisema Sima.

Alisema kufuatia changamoto hiyo alijenga hoja kwa kuomba shule mbili lakini aliambiwa atapewa fedha za shule moja hivyo aeleze zipelekwe wapi ambapo hakufikiria na kueleza zipelekwe kwenye kata hiyo ya Uhamaka.

"Niwashuru sana sehemu nyingine kumekuwa na changamoto kubwa ya ukamilishaji wa miradi ya Serikali fedha zinapelekwa lakini haikamiliki  ninyi hapa Uhamaka mmekuwa tofauti  mmeshiriki vizuri na kuhakikisha shule yenu imekuwa ya kiwango bora na ya mfano ambapo kila viongozi wamekuwa wakifika kuitembelea jambo ambalo najivunia mno," alisema Sima.

Wakati huohuo Sima aliwaomba wananchi wa Mtaa wa Ititi kuanza mara moja ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi kwa ajili ya wanafunzi na walimu kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo walimu hawana kabisa choo huku wanafunzi wakijisaidia kwa kusubiriana kutokana na kuwepo kwa choo kimoja tu.

Kwa wakazi wa Uhamaka aliwaambia waanze ujenzi wa Kituo cha Afya baada ya Zahanati inayotumika sasa majengo yake kuchakaa na kuwa na nyufa nyingi na kuelemewa kutokana na idadi kubwa ya watu ambao wanakwenda kupata huduma na kuwa ilijengwa miaka ya 1950 wakati watu wakiwa wachache.

"Nawaombeni anzeni ujenziwa maeneo haya mawili ili nikajenge hoja tuweze kuongezewa nguvu ya ujenzi kwani Serikali yetu ambayo ni sikivu chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani tunaweza kupatiwa fedha za kukamilisha ujenzi huo lakini kikubwa ni lazima na ninyi kuonesha mmeanza kufanya kazi hiyo kwa umoja na nguvu zenu," alisema Sima.

Akizungumzia suala la umeme alisema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Desemba 29, 2022 ilizindua mradi mpya wa kusambaza umeme kwenye Vijiji Miji viliyopo pembezoni mwa Manispaa ya Singida ambao utagharimu Sh. 7.11 Bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ndilo msimamizi wa mradi huo.

Alisema Kata ya Uhamaka ni moja ya mnufaika wa mradi huo wa kusambaza umeme katika Vijiji Miji (Peri-urban Electrification) na kuwaeleza wananchi hao wauchangamkie kwa kuanza kusuka  nyaya za umeme katika nyumba zao ili waweze kufungiwa kwa gharama ya Sh.27,000.

"Mradi huu ukikamilika unakwenda kubadilisha uchumi wa wanananchi kwani watautumia umeme huo kuanzisha viwanda vidogo  na shughuli zingine za uzalishaji ambazo zitatumia nishati hiyo hivyo kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla" alisema Sima.

Alisema hivi sasa tayari katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo nguzo zimekwishwa simikwa na kuwa mradi huo utaanza kufanya kazi wakati wowote.

Mbunge Sima akizungumzia kuhusu mkataba wa Bandari ya Dar es Salaam dhidi ya Kampuni ya DP World ya Dubai aliwata  wananchi wa kata hiyo kuwapuuza wale wote wanaotaka kupotosha ukweli wa mkataba huo wenye tija kwa nchi yetu kuwa eti Rais Samia Suluhu Hassan ameiuza bandari hiyo.

Alisema wabunge wasingeweza kuridhia kufanyika kwa maridhiano ya mkataba huo baina ya Tanzania na DP World iwapo kama kungekuwepo kwa viashiria vya kuuzwa kwa bandari hiyo.

Alisema kupitia uwekezaji huo Tanzania itakuwa ikipata Sh.Trilioni 26 kwa mwaka tofauti na sasa ambapo tunapata Sh.Trilioni 7 tu kupitia bandari hiyo kwa mujibu wa taarifa zilizopo.

Alisema hata hivyo suala hilo litazungumzwa kwa kirefu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo katika mkutano wa hadhara utakofanyika leo Viwanja vya Bombadia ambapo ataambatana na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho na wananchi watapata uelewa kuhusu jambo hilo.

Katika ziara hiyo Mbunge Sima alitembelea Shule ya Msingi ya Ititi na kujionea changamoto kubwa ya kutokuwa na vyoo ambapo pia alitembelea Shule ya Msingi ya Uhamaka na kuona baadhi ya madarasa yakiwa na nyufa jambo ambalo linahatarisha maisha ya wanafunzi.

Eneo lingine ambalo alitembelea ni Zahanati ya kata hiyo ambayo pia alikuta majengo yake yakiwa na nyufa huku mbao za paa lake zikiwa zimeoza,ambapo pia atembelea Shule Mpya ya Sekondari ya Uhamaka na alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi na kuwataka kuzingatia masomo na kufuata maadili yatakayo wafanya watimize ndoto za maisha yao.

Diwani wa Kata hiyo Senge M. Senge alipata fursa ya kuelezea miradi iliyokamilika na thamani yake na changamoto kadhaa zilizopo ikiwa ni pamoja na barabara ya kutoka katika kata hiyo na kuunganisha na barabara kuu ya kutoka Igunga kwenda Dodoma eneo la Ititi Manispaa ya Singida.

Mbunge Sima, akihutubia wananchi wa Kata ya Uhamaka baada ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi. 

Diwani wa Kata ya Uhamaka, Senge M. Senge (katikati) akimueleza Mbunge Sima changamoto ya uchakavu wa majengo ya Zahanati ya kata hiyo.
Mbunge Sima (aliyekaa jirani na kreti la soda katikati) akiwa amekaa na Wazee wa Mtaa wa Ititi wakibadilishana mawazo ya hapa na pale kuhusu maendeleo ya kata hiyo wakati wa ziara hiyo.
Muonekano wa choo kimoja wanachokitumia wanafunzi wa kike na kiume wa Shule ya Msingi Ititi na kuwafanya kujisaidia kwa kusubiriana jambo ambalo ni adha kwao.
Mbunge wa Singida, Musa Sima, akiangalia nyufa katika moja ya darasa katika Shule ya Msingi ya Uhamaka jambo ambalo linahatarisha usalama wa wanafunzi wanaolitumia darasa hilo ambalo jengo lake ni chakavu.
Muonekano wa jengo la utawala la Shule ya Sekondari ya Uhamaka baada ya ujenzi wake kukamilika.
Muonekano wa madarasa ya shule hiyo baada ya ujenzi kukamilika.
Diwani wa Kata ya Uhamaka, Senge M.Senge akiwa katika picha ya pamojanawanafunzi wa shule hiyo
Mbunge Sima akizungumza na wanafunziwa shule hiyo wakati wa ziarahiyo.
Mbunge Sima akisalimiana na wazee wa Kata ya Uhamaka walipokuwa kwenye kijiwe cha unywaji wa Kahawa.
Mbunge Sima akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata hiyo, John Gabriel ambaye hivi sasa anatoa huduma peke yake kufuatia wauguzi wawili wa zahanati hiyo kuwa nje ya kazi kwa sababu tofauti tofauti kwa zaidi ya miezi miwili sasa jambo linalomfanya akose muda wa kupumzika kutokana na kufanya kazi masaa 24.
Mbunge Sima akiwasalimia wakina mama wakati wa mkutano wakewa hadhara katika kata hiyo.
Wazee na Vijana wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanawake wakiwa kwenye mkutano huo.
Burudani ikitolewa na kikundi cha Sanaa cha wanawake wa kata hiyo.
Taswira ya mkutano huo.
Mwenyekiti Mstaafu wa Kata hiyo, Mzee Philemon Hango akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Uhamaka, Ally Rume, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, Mzee Ramadhani Bayu akizungumza katika mkutano huo.
Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Pili John Shashi, akiongoza mkutano huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Uhamaka, Mzee Juma Omari akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa kata hiyo, Senge M.Senge akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Vijana wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkazi wa kata hiyo, Moshi Juma akiuliza swali wakatiwa kumelezea Mbunge Sima kero mbalimbali.
Kero mbalimbali zikiwasilishwa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Uhamaka, Khalfan Ramadhan akimkabidhi Mbunge Sima zawadi ya kidumu cha lita tano cha asali, zawadi ambayo alikabidhiwa pia Diwani wa kata hiyo, Senge M.Senge ikiwa ni kutambua mchango waokatika kuiletea maendeleo kata hiyo.
Mbunge Sima akionesha zawadi hiyo baada ya kukabidhiwa.
Mkazi wa Kata hiyo, Mwalimu Mstaafu, Daniel Kanka Senge, akimshukuru Mbunge Sima kwa kazi kubwa anayoifanya ya kupeleka maendeleo katika kata hiyo. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: