Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Chatanda amemshukia vikali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe kwa kile alichokieleza kuwa amekosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimtoa gerezani alikokaa kwa muda mrefu tangu kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mikoa ya Kusini mwa Tanzania Chatanda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, hivi karibuni Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akimtukana Rais Samia kwa kueleza kuwa ameuza nchi jambo ambalo halina usahihi na linachonganisha Wananchi, hivyo kutoa wito kwa Wananchi hao kuwapuuza na kutowasikiliza pale watakapoitisha mikutano yao.

"Anazungumza, anamtukata, anasema ameuza nchi, kwani sisi tumeuzwa hapa tulipokaa?, Kuna mtu anayesema kuwa nimeshawanunua ninyi ni watu wangu?, Wakija msiwasikilize.., anasema anaenda kujiandaa mikutano 70..."
Ameendelea kueleza kuwa kinachotokea kwa Mbowe sasa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi.
Share To:

Post A Comment: