Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa H. Aweso (Mb) ametengua uteuzi wa Meneja wa Maji Mkoa wa Dodoma, (RUWASA) Mhandisi Godfrey Kabula Mbabaye kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Waziri Aweso amechukua hatua hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019,

Aidha, Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba kuunda timu ya Wataalam ya kufuatilia changamoto ya utekelezaji wa Miradi ya Maji kwa Mkoani Dodoma na kutoa suluhisho la kumaliza changamoto hizo mara moja.

Vilevile, ameelekeza timu hiyo ya Wataalam itakayoundwa na katibu Mkuu ifanye tathimini ya utendaji kazi wa Mameneja wa Wilaya zote wa Maji Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma.
Share To:

Post A Comment: