Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya Dunia yatakayofanyika kitaifa Jijini Arusha mnamo Juni 26, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John K V Mongella amesema Rais Samia atahudhuria katika maadhimisho hayo ya siku ya kupambana na kupiga vita madawa ya kulevya hapa nchini yatakayo fanyika Juni 25, 2023 siku ya Jumapili katika viwanja vya Shehk Amri Abeid.

Mongela ameeleza kuwa dawa za kulevya zinaleta athari kubwa kwa jamii na zina takiwa kupingwa kwa nguvu zote ili kunusuru vizazi vijavyo kwa maendeleo ya taifa la Tanzania ili kuwa na nguvu kazi za kulijenga taifa kiuchumi.

"Maadhimisho haya ambayo kauli mbiu yake ni "Zingatia utu, kuimarisha Huduma za Kinga Tiba", Lengo lake kubwa ni kuhakikisha kila jamii ipige vita dawa za kulevya wakiwemo viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kupiga vita matumizi ya madawa hayo yanayoleta athari kwa jamii sambamba na kurudisha nyuma maendeleo ikiwemo uchumi wa familia na Taifa". Amesema Mongela.

Aidha Mongela alitoa rai kwa viongozi na jamii nzima ni lazima wawajibike ili kudhibiti janga la matumizi ya dawa za kulevya na kusisitiza kila mtu awajibike kuchukua hatua dhidi ya dawa za kulevya kwani kunabaadhi ya waathirika hupelekea kuwa wahalifu hivyo lazima kuungana kwa pamoja katika kudhibiti vita hii ya kupambana na dawa hizo.

"Vita ni vita jambo la dawa za kulevya na biashara ya dawa za kulevya ni janga na walioingia katika matatizo haya yanaonekana haswa katika ngazi za familia zetu yatupasa kugina sote maana athari za madawa haya ni makubwa mmo kwa jamii ni waombe viongozi wenzangu, viongozi wa dini na jamii sote kuwa wamoja katika vita hii ili kulinusuru vijana wetu". Ameongeza mongela.

"Serikali inafanya kazi kubwa za kuanzisha vituo vya urekebishaji wa tabia na tiza za warahibu wa madawa ya kulevya (soba house ) ambavyo vinatoa huduma za dawa kwa warahibu mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuwanusulu wale ambao wamesha athirika na mada hayo ili waweze kulitumikia taifa kwa namna moja au nyingine". Aliongeza mongela.

Kwa upande wao viongozi wa dini na mila Mkoa wa Arusha wameeleza kuwa jambo la kupambana na madawa ya kulevya ni jukukumu la kila mtu moja moja na siyo la serikali peke yake na viongozi wa dini.

"Ni muda sasa umefika kwa watanzania kuinuka na kuipambania nje yao wenyewe na kukataa yale yote ambayo hayafai katika jamii zetu maana watumiaji wa madawa ya kulevya wakizidi jamii zetu pia haziko salama maana uhalifu utazidi ikiwemo matendo ya wizi na ubakaji". Alisema Gulaam, mmoja wa viongozi wa dini.

Nae Laigwanani Mkuu wa Kabila la Maasai nchini Tanzania Olekisongo Meijo amesema kuwa kwa wale wote wanao husika na uuzwaji wa madawa ya kulevya wachukuliwe hatua kali ili kuwa fundisho wa wengine ambao wanafanya biashara hiyo ambayo inapelekea kupoketa vijana ambao ni tegemezi kwa familia na taifa.

Hata hivyo ikumbukwe Maadhimisho hayo yatafanyika viwanja vya Sheikh Amri Abeid na yatatanguliwa na maonesho ya wadau mbalimbali wanaopinga matumizi ya dawa hizo za kulevya Juni 23 ,2023 na kufikia kilele cha kitaifa yatakayo hudhuliwa na Rais Samia Juni 25, 2023.

Share To:

Post A Comment: