Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), Kata ya Manyoni wakiandamana maandamano ya amani ya kupinga ukatili wa kijinsia, ushoga na usagaji yaliyofanyika mjini Manyoni jana. Maandamano hayo yameandaliwa na SMAUJATA Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Na Dotto Mwaibale, Manyoni

SHUJAA wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wamefanya maandano ya amani ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ushoga na usagaji kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii iweze kuachana na vitendo hivyo ambavyo vinakiuka maadili ya kitanzania.

Maandamano hayo  yalianzia Sheli ya Ridhiwani, Hospitali ya Wilaya na Majengo ambapo ilitolewa elimu ya kupinga ukatili sanjari na kuchangia damu salama.

Diwani wa Kata ya Manyoni, Saimoni Mapunda akizungumza baada ya kupokea maandamano hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema maandamano hayo ni ya muhimu katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wilayani humo.

Alisema maandamano hayo yalioratibiwa na SMAUJATA na kuambatana na zoezi hilo la uchangiaji damu salama lililoongonzwa na Mtaalam wa damu Kucy Kibaja kutoka Hospitali ya Benjamini jijini Dodoma yalilenga kupinga vitendo vya ukatili, ndoa za jinsia moja (ushoga) , usagaji na ukatili wa aina mbalimbali.

Ili kupanua wigo wa mapambano hayo Mapunda aliwataka SMAUJATA kutoka ofisini na kwenda kwenye mikusanyiko ya watu kutoa elimu ya kupinga ukatili huo wa kijinsia.

"Nawaomba sio kukaa eneo moja bali nendeni walipo wananchi mkatoe elimu hiyo ya kupinga ukatili tena bila ya kuona aibu na kuelezea kazi zinazofanywa na SMAUJATA ili wazielewe," alisema Mapunda.

Mapunda aliipongeza SMAUJATA kwa kazi kubwa wanayoifanya katika wilaya hiyo ambayo siku za hivi karibuni ilichafuka kutokana na kuwepo kwa matukio ya mauaji yakiambatana na ufukuaji wa makaburi.

Mtaalam wa damu salama kutoka Hospitali ya Benjamini Kucy Kibaji alisema suala la uchangiaji wa damu ni la muhimu kwani inasaidia kuwaongezea majeruhi wa ajali, wajawazito wanapojifungua.

Alisema mbali ya kusaidia makundi hayo hivi sasa wanatibu watoto wenye sikoseli ambao wanatumia damu nyingi kwa kuchukua uroto kutoka kwa watu wa karibu yao ambao wamezaliwa sehemu moja na kuwa changamoto hiyo haipo kabisa.

Alisema watafanikiwa kuwasaidia watu wenye changamoto hiyo kwa jamii kuchangia damu kwa wingi kwani mtoto mmoja ili kufanyiwa matibabu na kupona anahitaji  chupa za damu 40.

Katika kusanyiko hilo mada kubwa iliyotolewa ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia na umuhimu wa jamii kuhusu uchangiaji wa damu.

Watoa mada hao waliongelea kuhusu kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili katika jamii ambapo waliwaomba, wazazi na  walezi kuwa jirani na watoto wao na kusimamia malezi yao wakiwa shuleni na nyumbani kwani imebainika wanaowafanyia ukatili huo wengi wao ni ndugu zao wa karibu.

Walisema ndoa kuvunjika pia kumechangia kwa kiasi kikubwa watoto kukosa matunzo na uangalizi mzuri na kujikuta wakiingia mitaani ambako wanafanyiwa vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kulawitiwa, kubakwa, ndoa za utotoni na mambo mengine mengi.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni katika maandamano hayo, Diwani wa Kata ya Manyoni, Saimon Mapunda, akihutubia baada ya kupokea maandamano hayo.
Mashujaa wa SMAUJATA wakiwa kwenye maandamano hayo.
Sheikh Hassan Omary Waziri akizungumza kwenye maandamano hayo
Mashujaa wa SMAUJATA wilayani humo wakiwa katika kazi hiyo
Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Manyoni, Tatu Ramadhan akizungumza kwenye maandamano hayo
Katibu wa SMAUJATA Wilaya ya Manyoni, Napegwa Jared akizungumza.
Mwenyekiti wa SMAUJATA  wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hadija Kaherewa akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa SMAUJATA, Manispaa ya Singida, Hawa Ntandu akizungumza.
Mkutano ukiendelea.
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Manyoni, Lilian Likwelile, akizungumza.
Mashujaa wakiwa kwenye maandamano hayo.
Mashujaa wakiwa kwenye maandamano hayo
Mashujaa wa SMAUJATA, wa Kata ya Manyoni, wakiwa kwenye mkutano huo.
Mashujaa kutoka Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Ikungi, akizungumza kwenye mkutano huo.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakiwa kwenye mkutano huo.Kutoka kulia ni Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Nkonko, Rehema Chuji, Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kintinku, Joyce Kalikawe, Diwani Viti Maalum, Kata ya Manyoni, BlandinaMawalla na Diwani wa Kata ya Manyoni, Saimon Mapunda.
Mkuu wa Polisi Kata ya Manyoni, A/Insp, Mwinyange akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Manyoni, Juma Amrani akiongoza mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA, Wilaya ya Manyoni, Tatu Ramadhan, akimkabidhi risala mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, katika maandamano hayo, Saimon Mapunda.
Makamu Mwenyeki wa SMAUJATA Kata ya Manyoni, Wallece Shechambo akizungumza kwenye mkutano huo.Mtaalamuwa Damu salama kutoka Hospitali ya Benjamini Dodoma, akizungumza kwenye mkutano huo.


Uchangiaji damu ukiendelea.
Katibu wa SMAUJATA Kata ya Manyoni, Sarah Yohana, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Taswira ya mkutano huo.
Mashujaa wa SMAUJATA wakiwa kwenye kikao baada ya mkutano huo.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: